July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sakata la Mwalimu Mkuu kushushwa cheo lachukua sura mpya

Spread the love

SAKATA la aliyekuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi, Mtoni Kijichi, Evelyne Munisi iliyopo Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam limechukua sura mpya, baada ya wazazi wa shule hiyo kuadhimia kumuita Mbunge, Mkuu wa Wilaya na Meya kwenye kikao kinachotarajiwa kufanyika Jumamosi kwa lengo la kupata ufumbuzi wa tatizo hilo. Anaripoti Mwandishi wetu… (endelea)

Huku, diwani wa Kijichi, Eliasa Mtarawanje akituhumiwa kuwatishia wazazi wa shule hiyo kupitia kwa Katibu wa Kamati ya Wazazi, Mathias Balijuza kuwa endapo watafanya mkutano shule hapo, atawafunga.

Akizungumza katika mkutano huo, ambao ulifanyika jumamosi nje ya chumba cha darasa la VII A, Bulijuza alisema kuwa alitishiwa kufungwa na diwani huyo, baada yakutaka  kuwatangazia wanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo, wawaambie wazazi wao waje kwenye kikao ambacho kilifanyika jumamosi shule ni hapo.

“Alinitishia Balijuza, Balijuza nitakufunga, nitakufunga wewe unataka kuleta fujo kwenye eneo la shule, angalia nitakufunga, picha hiyo ilinichanganya ikabidi niwapatie wazazi taarifa ya mkutano kupitia ujumbe wa simu.

“Baadhi ya wazazi kusikia hili tishio, walihofia kufika kwenye kikao hichi cha wazazi, kwa sababu mimi nilikwenda kutoa taarifa kwa niaba ya wazazi wote,” alisema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Butiama, Kata ya Kijichi, Haji Mgaya alisema amepata mualiko kupitia Kamati ya Shule kwa ajilinya kuangalia mchakato mzima wa elimu bure, lakini alipofika katika mkutano huo alikutana na changamoto nyingi ikiwemo ya Mwalimu kushushwa na madarasa yanayifanyiwa  mikutano yamefungwa.

“Ninachokiomba wananchi wote katika eneo langu kwa kuwa maadhimio yetu ni kuangalia tatizo lililopo katika mchakato wa elimu hadi mwalimu  kushushwa daraja naomba mjitokeze kwa wingi katika mkutano utakaofanyika jumamosi”,

” Niwatoe hofu wazazi, sisi na Kamati ya wazazi tunasimamia sheria, hakuna taasisi yoyote ya kipolisi inayoweza kufanya jambo kinyume na taratibu na sisi tupo kwenye miongozo ndiyo maana tunaalika watu wenye sifa kuja kutoa maamuzi

Alisema mkutano huo umeadhimia kuwaita viongozi hao ili kuja kutatua mgogoro uliopo ndani ya shule ya Msingi Mtoni Kijichi baina ya Kamati ya Wazazi, Mwalimu na diwani wa kijichi.

Kuhusiana na kufungwa kwa milango la madarasa, Kaimu Mkuu wa shule hiyo, Twaha Kifunde alisema madarasa hayo yalifungwa kama kawaida na walinzi, kwa sababu hakukuwa na mkutano rasmi shuleni hapo na mtu wa kwanza kutangaza mkutano ni Mwalimu Mkuu.

“Hakuna aliyeniambia nimfungulie vyumba vya madarasa nikakataa na hii taarifa ya kuwa mimi nipewa maelekezo na diwani ya kukataza mkutano usifanyike shuleni hapa si za kweli, kwa sababu kuna utaratibu wa kufanya mikutano,” alisema Mwalimu Kifunde

Akijibu tuhuma hizo, Diwani Mtarawanje alisema hayo ni mambo ya kisiasa tuachanenayo, kwa sababu yeye anasimamia Serikali kutokuchangisha wazazi michango ya shule kwa sababu, Serikali inatoa elimu bure.

“Haya mambo siyataki kuyasikia, sisi tunasimamia Serikali kutokuchangisha michango, mambo ya kupigiana pigiana simu sio, waache na tuhuma zao.Tuhuma zao zingine ni zipo? achana nazo hizo habari, mambo ya kisiasa hayo achana nayo,” alisema Diwani Mtarawanje

Hayo yote yametokana na  kikao cha wazazi kilichokaa kupitisha maadhimio kuwa kila mzazi mwenye mtoto wa darasa la sababu achangie Sh 8,000 kwa ajili ya masomo ya ziada, ambapo badae Mwalimu Munisi alishushwa daraja na kuwa Mwalimu wa kawaida kwa madai kuwa yeye ndiye alichangisha michango h

Alisema mchanganuo wa fedha hiyo ni kwamba , Sh 10,000 ni ya chakula cha mchana kwa wanafunzi hao, ambapo sahani ya chakula kwa siku ni sh 500 na Sh 5000 iliyobaki ni kwa ajili ya gharama ya uchapishaji wa mitihani ya masomo matano ambayo yatakuwa yanafanyika kila jumamosi ya wiki.

 

error: Content is protected !!