February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sakata la MO, Manara akamatwa

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa

Spread the love

HATUA ya Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kusambaza habari za kutekwa kwa Mohammed Dewji (MO) kwa madai ya kutumwa na familia, sasa inamtokea puani. Anaandika Mwandishi Wetu … (endelea).

Tayari Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa kwa Manara.

Kamanda Mambosasa amesema, Manara anashikiliwa kutokana na kusambaza taarifa za tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii kwa madai ya kutumwa na familia, lakini sio kweli

“Manara tunamshikilia kwa uchunguzi zaidi yeye amekuwa akisambaza taarifa mbalimbali za tukio hili kwenye mitandao ya kijamii kwa madai kuwa ametumwa na familia, lakini sio kweli, hajatumwa na familia hivyo tunamshikilia,” alisema Kamanda Mambosasa.

Mapema jana Manara alinukuliwa akiwataka akisema taarifa ya MO kupata matatizo imemshtua kila mmoja na kwamba bado wanaliachia jeshi la polisi kufanya kazi ya kumpata mwekezaji wao.

“Wanasimba wawe watulivu wakiliachia jeshi la polisi kufanya kazi yake na kwamba wanaamini MO atapatikana akiwa hai,” alisema Manara.

error: Content is protected !!