
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ameingia kigugumizi kuzungumzia ukimya uliomshtua Rais John Magufuli. Anaripoti Mwandishi wetu … (endelea).
Badala yake ametaka waandishi wa habari kumuuliza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro kwa kuwa alikuwepo Ikulu wakati Rais Magufuli akihoji.
Rais Magufuli alionesha kushangazwa na Jeshi la Polisi kuendeleza ukimya juu ya kutekwa na kupatikana kwa mfanyabiashara bilionea Mohammed Dewj (MO).
Kiongozi huyo wa nchi wakati akiwaapisha mawaziri wawili Ikulu jijini Dar es Salaam alisema, Watanzania sio wajinga na walitarajia kujua nini kinaendelea lakini Jeshi la Polisi limekaa kimya.
Kamanda Mambosasa alipozungumza na waandishi wa habari leo tarehe 7 Machi 2019, anaizungumziaje kauli ya Rais Magufuli kuhusu kutekwa, kukamatwa na ukimya unaoendelea.
Swali hilo Kamanda Mambosasa hakuwa tayari kulijibu na badala yake alisema, Amiri Jeshi Mkuu akizungumza, jeshi linatekeleza.
“Aliongea ni Amiri Jeshi Mkuu, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama na sisi tumefundishwa, Amiri Jeshi akiongea hakuna majadiliano, hakuna ufafanuzi. Tumelipokea na linafanyiwa kazi,” alisema Kamanda Mambosasa.
Hata hivyo Kamanda Mambosasa alirudisha swali hilo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kwamba, alikuwepo hivyo anaweza kujibu.
“Wakati linatolewa tamko hilo IGP alikuwepo, msemaji wa jeshi yupo anaweza akaulizwa” amesema Kamanda Mmbosasa.
Ikumbukwe tarehe 4 Machi 2019 Rais Magufuli aliibua maswali tata juu ya utendaji kazi wa Jeshi la Polisi katika tukio la kutekwa MO.
Alisema, wanapaswa wajue watanzania wanahitaji kujua kinachoendelea
Rais Magufuli alieleza kuwepo kwa mkanganyiko wa maelezo ha polisi Kutokana ikiwa ni pamoja na kuwa MO alitekwa na wazaungu, mara alietekwa kaonekana kwenye viwanja vya Gymkhana huku watu wakijiuliza alifikaje huko.
Na baadaye jeshi hilo la polisi likaja kuonesha nyumba alipokuwa amewekwa MO baada ya kutekwa.
Mara mtu aliyekuwa akiwabeba watekaji hao akaoneshwa lakini hakufikishwa mahakamani mpaka hivi sasa.
Rais Magufuli aliongezea kuwa, Watanzania walitaka kujua hatua ambazo Jeshi la polisi ilizichukua kwa watu waliokamatwa wakihusishwa na tukio hilo.
Tazama video kamili hapo chini
More Stories
Barrick ilivyoshiriki katika kuadhimisha Siku ya Canada
PURA yaanzisha kanzidata
Branch kufikisha mikopo ya haraka kwa mamilioni ya Watanzania