Sunday , 26 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Sakata la Mdee, wenzake: Prof. Safari, Lissu watofautiana
Habari za SiasaTangulizi

Sakata la Mdee, wenzake: Prof. Safari, Lissu watofautiana

Spread the love

 

WAKATI Tundu Lissu, Makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akieleza chama hicho ‘kujivuwa’ kuwapeleka mahakamani Halima Mdee na wenzake, Prof. Abdallah Safari, Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa chama hicho amesema ‘muafaka unapatikana mahakamani.’ Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Lissu hivi karibuni ameeleza, kwamba chama hicho kamwe hakitakwenda mahakamani kuwashitaki Mdee na wenzake kupinga ubunge wap kupitia chama hicho, na kwamba wanakwenda kuwashitaki kwenye mahakama za umma.

”Hatutakwenda mahakamani, tutapambana kwenye mahakama ya umma wa Watanzania na Mahakama ya Umma ya Jumuiya ya Kimataifa, uwanja wa mapambano ni kubwa sana,” amesema Lissu tarehe 5 Februari 2021, kwenye mahojiano ya moja kwa moja na kituo kimoja cha habari za mtandaoni.

“…kitu ambacho kiko ndani ya mamlaka ya chama ni kuwafukuza uanachama, kujulisha hizo mamlaka za kikatiba kwamba si wanachama wa Chadema,” alisema Lissu ambaye aligombea urais kupitia chama hicho Tanzania Bara na kushika nafasi ya pili.

Hata hivyo, Prof. Safari ambaye ni gwiji wa sheria nchini amesema, angekuwa kiongozi wa Chadema sasa, angekuwa ameishawafikisha mahakamani Mdee na wenzake 18.

Amesema, mahakama ndio chombo sahihi cha kumaliza utata kati ya pande mbili zinazokinzana kuhusu uhalali wa Mdee na wenzake kuapishwa na kuwa wabunge wa Viti Maalumu licha ya kutimuliwa uanachama na uongozi wa Chadema.

Mdee na wenzake walifukuzwa uanachama baada ya kukiuka msimamo wa chama hicho wa kutotambua matokeo ya uchaguzi mkuu 2020, na kugoma kuteua wabunge ili kushiriki vikao vya Bunge la Jamhuri. Mdee na kundi lake walikiuka msimamo huo na kujipeleka bungeni.

“Ningekuwa kongozi Chadema, saa hizi zamaani nginekuwa (nimewapeleka) mahakamani,” amesema Prof. Safari wakati akizungumza na televisheni moja ya mtandaoni tarehe 8 Februari 2021.

Prof. Safari ambaye ni Makamu Mstaafu wa Chadema amesema, suala la Mdee na wenzake lingeweweza kuisha haraka iwapo Chadema wangekwenda kuomba tafsiri ya kikatiba kuhusu uhalali wa Mdee na wenzake kuwa wabunge licha ya kutimuliwa uanachama.

“Kuna njia moja muhimu ya kufanya, Chadema kuwashtaki hawa kwa sababu mwenye mamlaka ya kusema na kusikilizwa ni vyombo vya dola, kwamba hawa ni wabunge halali ama si halali sio Ndugai (Spika Job Ndugai), wala sio Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi wala sio sisi Chadema.

“Mwenye mamlaka ya kufanya hivyo ni mahakama, kwa hiyo mahakama inaombwa kwa kuwa ni ya Kikatiba, itakuwa na majaji watatu, inaombwa ilete tafsiri sahihi hawa wabunge kwa mujibu wa Katiba ni wabunge ama si wabunge,” amesema.

Mwanasheria huyo amesema, si wanasheria wala Spika Mstaafu, Piusi Msekwa wanaweza kusadiki kwamba, Mdee na wenzake wanaweza kuwa wabunge bila kuwa na chama.

“Kuna watu wamesema hawa si wabunge, Mzee Msekwa, wanasheria wote wanasema hawa si wabunge, Ndugai anasema ni wabunge, wapi? Ubishi unamalizwa kule mahakamani. Mahakamani ndio msema kweli,” amesema.

Chadema kupitia Kamati Kuu yake iliyoketi tarehe 27 Novemba 2020, iliwavua uanachama Halima Mdee na wenzake 18 kwa kukiuka umauzi wa chama hicho na kwenda kuapishwa bungeni kuwa wabunge wa viti maalumu.

waliotimuliwa Chadema ni Mdee mwenyewe, Ester Bulaya, Esther Matiko, Nusrat Hanje, Grace Tendega na Hawa Mwaifunga.

Wengine ni Jesca Kishoa, Agnesta Lambat, Tunza Malapo, Ceciia Pareso, Asia Mwadin Mohamed, Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Siyao, Salome Makamba, Anatropia Theonest na Conchesta Lwamlaza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!