June 19, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sakata la Mazrui lachukua sura mpya: ACT-Wazalendo waishitaki Polisi

Nassor Ahmed Mazrui, Naibu Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo Zanzibar

Spread the love

CHAMA cha siasa cha ACT- Wazalendo, nchini Tanzania, kimengua shauri Mahakama Kuu ya Zanzibar, kutaka mahakama hiyo, kutoa amri ya kufikishwa mahakamani au kuachiwa huru kwa mmoja wa vigogo wandamizi wa chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Mwanasheria mkuu wa chama hicho, Omar Said Shaaban amesema, kesi hiyo imefnguliwa leo mjini Unguja. Amewataja washitakiwa kuwa ni Naibu Mkurugenzi wa Upepelezi wa makossa ya jinai Zanzibar (DCI) na Kamishena Mkuu wa Polisi Visiwani.

“Baada ya maofisa wa polisi Zanzibar kushindwa kutueleza waliko baadhi ya wanachama wetu, leo nimefungua shauri mahakama kuu ya Zanzibar, kuomba mahakama hiyo imuagize kamishena wa polisi na DCI waachie huru au wawalete mahakamani,” ameeleza.

Miongoni mwa viongozi wa ACT- Wazalendo wanaodaiwa kushikiliwa na polisi, ni pamoja na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui.

Mwanasiasa huyo shupavu na roho ya uhai wa chama hicho, anadaiwa kukamatwa katika maandamano ya amani yaliyoitishwa na mwenyekiti wake, Maalim Seif Shariff Hamad, kupinga uchaguzi mkuu wa Zanzibar. Mpaka sasa, hajaweza kukutana na familia yake wala mawakili wake.

Mazrui ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ushindi ya kampeni za Maalim Seif, alifikwa na dhahama hiyo, takribani siku tatu tangu aliporipotiwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana kufuatia gari lake kugongwa eneo la Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU).

Inadaiwa baada ya tukio la kugongwa, watu ambao hawafahamiki walimkamata na kutokomea naye kusikojulikana.

Tukio hilo limetokea asubuhi hii ya Jumapili, tarehe  25 Oktoba, eneo la Saateni wakati akielekea katika ofisi za makao makuu ya ACT-Wazalendo zilizopo Vuga.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Awadh Juma Haji, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. Alisema, jeshi hilo linaendelea na uchunguzi.

“Uchunguzi ukikamilika tutatoa  taarifa zaidi.Kwa sasa siwezi  kulielezea kwa urefu tukio hilo ila ni kweli tumepokea taarifa hizo tumeshaanza kuzifanyia kazi,” amesema Kamanda Haji.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, makao makuu ya ACT-Wazalendo, jijini Dar es Salaam, Zitto Kabwe, kiongozi mkuu wa chama hicho amesema, mpaka jana ikiwa ni siku ya 12 tangu kukamatwa kwa Mazrui, hakuna taarifa rasmi ya wapi anakoshikiliwa.

Alisema, katika mazungumzo yake na baadhi ya viongozi wa polisi wamethibitisha kumshikilia mwanasiasa na mfanyabiashara huyo, lakini akaongeza, “hatujapata nafasi hata ya kumuona.”

error: Content is protected !!