September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sakata la Malasusa, watoto watoroshwa

Spread the love

MUME wa mwanamke anayedaiwa kumkamata ugoni Askofu Dk Alex Malasusa wa Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania (KKK) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, (DMP) anatafuta watoto waliotoroshwa kwa maelekezo ya Malasusa na Jeshi la Polisi, anandika Josephat Isango.

Akizungumza na MwanaHALISI online baada ya kuachiwa huru kutoka polisi kwa tuhuma za kushambulia, amesema watoto wake walichukuliwa na raia mmoja mjerumani aliyeolewa na mtanzania, anaitwa Caroline Shedafa.

Caroline Shedafa ametuhumiwa kuwa ametumia mwanya wa malalamiko ya Mwakilima na Malasusa kwa sababu ya urafiki alifanikiwa kuwatorosha watoto hao na kwamba ana mpango wa kuwasafirisha kwenda nje ya nchi wakati wowote.

MwanaHALISI limemtafuta Shedafa kwa tuhuma hizo, alipokea simu na baada ya kuambiwa kuwa anaongea na MwanaHALISI alikata simu na kukataa kuongea suala hili na mwandishi.

Malasusa anadaiwa kuwa anadaiwa kushirikiana na mfanyakazi wa hospitali ya Muhimbili anayeitwa Julieti, aliyewaambia ndugu wa mume anayenyang’anywa mke wake na malasusa kuwa atakiona.

“Huyu kaka anajidai mjuaji, hapti kitu, utaratibu uko tayari wa kuwasafirisha watoto kwenda nje ya nchi na hatawaona tena, ataishia kuwasikia tu, mimi ni mtu wa Karibu na Askofu Malasusa ndo nawaambia”. Alinukuliwa dada huyo akiongea kwa ujasiri.

Hadi sasa watoto wanaotafutwa na baba yao ambao Jeshi la Polisi linadaiwa kushirikiana na Malasusa licha ya taarifa zao kufika polisi kituo cha Wazo na kutochukuliwa hatua ni Sijenuni, Sephania, na Simon wote wanadaiwa kuwa watoto wa Venance Mwakilima.

Taarifa za leo usiku zilizofikiwa MwanaHALISI online zinadai kuwa baadhi ya Maaskofu Jijini Dar es Salaam wameamua kujitokea kulinda heshima ya uaskofu baada ya kudhalilishwa na Malasusa.

Maaskofu ambao hawakupenda kutajwa majina yao kwa kuwa si wasemaji wa vikao halali wamesema “hili suala tunalichukua,

Malasusa ana tuhuma nzito nchini, na baada ya gazeti kuandika watu wamejitolea kujieleza tunaomba muda kesho (Jumanne) tutaliongelea hadharani baada ya kukutana na mume wa me.

Aidha Malasusa hakupatikana kwenye simu zake wala kujibu ujumbe wa simu aliotumiwa tangu juzi wakati gazeti la MwanaHALISI likiendelea kufuatilia sakata hili.

Taarifa ambazo mwandishi anazo zinadai viongozi wakubwa wa serikali wanaingilia suala hili, zinafuatiliwa na zitaandikwa kwenye gazeti la MSETO…

error: Content is protected !!