Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sakata la makinikia laibuka bungeni
Habari za SiasaTangulizi

Sakata la makinikia laibuka bungeni

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Spread the love

 

MBUNGE wa Msalala mkoani Geita (CCM), Idd Kassim, amesema usafirishaji makontena ya makinikia kutoka Mgodi wa Bulyanhulu, umezua taharuki kwa wananchi , wakihofia kurudi kwa vitendo vya utoroshaji michanga ya madini ya dhahabu. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).

Kassim ametoa kauli hiyo leo Jumatano, tarehe 3 Juni 2021, katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, bungeni jijini Dodoma.

Mbunge huyo wa Msalala amehoji, kwa nini makontena hayo yanasafirishwa wakati Serikali ilipiga marufuku usafirishaji makinikia.

“Tunatambua ya kwamba, Serikali ilizuia kabisa usafirishaji makinikia nje ya nchi na sasa tumeshuhudia makontena ya makinikia yakisafirishwa, kupitia Barabara ya Bulyanhulu, kwenda Kahama na Bandari yetu ya Dar es Salaam,”

“Na kupelekea taharuki kwa Watanzania na kwa wananchi Msalala, Nini kauli ya Serikali kuhusu jambo hili?” amesema Kassim.

Sakata la kuzuiwa kwa makontena zaidi ya 200, yaliyokuwa na mchanga wa dhahabu kwenye Bandari ya Dar es Salaam, kuelekea nje ya nchi, liliibuka mwaka 2017.

Baada ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli, kubaini udanganyifu wa viwango vya madini yaliyomo ndani yake, kitendo kilichoikosesha mapato Serikali.

Hata hivyo, mwanzoni mwa 2020, Magufuli aliruhusu makontena hayo yasafirishwe baada ya kuzuiwa kwa zaidi ya miaka miwili. Hatua iliyochukuliwa kufuatia mabadiliko ya sheria, yaliyosababisha uundwaji wa Kampuni ya Madini ya Twiga, kati ya Serikali na Kampuni ya Madini ya Barrick.

Akizungumzia sakata hilo, Waziri Majaliwa alisema makontena hayo hayatoroshwi kwani Serikali imeweka utaratibu mpya.

Waziri Majaliwa amesema utaratibu huo mpya, ni wa kuchunguza mchanga uliomo kwenye makontena pamoja na kuuzwa kabla hayajasafirishwa nje ya nchi, ambapo Serikali inapata mgawo wake.

“Kwanza kupitia wataalamu, baada ya kuchimbwa tunapitia kujua aina zote za madini. Mwanzo tuliambiwa kuna aina moja ya madini ya dhahabu, lakini kumbe kule ndani baada ya ukaguzi tumegundua tuna aina tano za madini,” amesema Waziri Majaliwa.

Waziri Majaliwa amesema “leo hii kupitia kampuni zetu, Serikali inauza madini yote matano na sio moja kama zamani. Tukigundua aina zote tunauza ndani ya nchi na sio nje ya nchi. Makontena yanayosafirishwa tayari yameshauzwa na Serikali imeshapata fedha yake na imeshahifadhiwa kwenye akaunti zetu.”

Waziri Mkuu huyo wa Tanzania amesema, kwa sasa Serikali imeruhusu usafirishwaji wa makontena hayo, baada ya kuanzishwa kwa utaratibu huo mpya.

“Kwa hiyo Watanzania hatupati hasara, yakishauzwa hatua inayofuata mnunuzi anakua huru kuyapeleka anakotaka na ndio hayo mnayoona yakipita. Nataka niwaondoe hofu kuwa, makontena hayo yameshauzwa, na huyo ni mnunuzi na waondoe mashaka juu ya usafirishaji wa kontena yenye makinikia,” amesema Waziri Majaliwa.

Aidha, Waziri Majaliwa amesema, timu za uchunguzi wa makinikia ziko kuanzia migodini hadi katika Bandari ya Dar es Salaam.

“Sababu Serikali iko makini sana inayotimu ya uhakiki kwenye mgodi, lakini pia timu ya kuhakiki mauzo kuhakikisha fedha inalipwa. Hakuna kontena linatoka nchini bila ya kuuzwa , lakini tumeweka timu pale bandarini kuhakikisha kila kontena la makinikia linaloingia pale, lina nyaraka zote za manunuzi,” amesema Waziri Majaliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!