Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Habari Siasa Sakata la Lissu: Wabunge CCM wamlalamika Ndugai
SiasaTangulizi

Sakata la Lissu: Wabunge CCM wamlalamika Ndugai

Job Ndugai, aliyekuwa Spika wa Bunge Tanzania
Spread the love

BAADHI ya wabunge kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameeleza kutofurahishwa na kitendo cha Job Ndugai, Spika wa Bunge kumvua ubunge Tundu Lissu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Wakizungumza kwa sharti la kutoandikwa majina yao, wabunge waliozungumza na MwanaHALISI ONLINE wameeleza kuwa, kilichofwanywa na Spika Ndugai kinastaajabisha.

Wameeleza kwamba, Bunge na kila Mtanzania (akiwemo yeye) wanajua Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki, yupo kwenye matibabu nje ya nchi.

“Hakuna unachoweza kusema kuhusu Lissu kuvuliwa ubunge isipokuwa chuki,” ameeleza mbunge mmjoka kutoka Kanda ya Ziwa akifafanua kwamba, “ni Mtanzania yupi ambaye anaweza kupuuza maisha ya Lissu yaliyoponea kwenye tundu la sindani?”

Mbunge huyo amesema kuwa, Tanzania inapaswa kuhama kwenye siasa za chuki pia kutumikishwa na kwamba, Singida Mashariki ilimchagua Lissu kwa kura nyingi kwa kuwa, wanamwamini.

“Unajua haya yanatokea kutokana na Watanzania tulivyo, nadhani ilikuwa jambo la busara sana kuhakiki afya la Lissu kabla ya fikra za kisiasa kupewa kipaumbele. Tunapaswa kuzingatia dunia hii tunapita,” amesema.

Mbunge mwingine wa chama hicho kutoka Kanda ya Kaskazini amesema kuwa, tayari uchaguzi katika Jimbo la Singida Mashariki umetangwaza na kwamba, bila shaka CCM itashinda.

Amesema, hata CCM ikishinda hakuna cha kujivunia kwa kuwa, chama hicho kitakuwa kimepora ubunge wa mtu ambaye ni mgonjwa kwa kulitumia Bunge.

“Hakuna asiyejua madhira yaliyompata Lissu. Lissu alipigwa risasi mchana kweupe kabisa na akiwa anatokea katika majukumu yake, hakuna asiyejua alipo. Sasa hata ukishinda, unawezaje kujisifu? Ninachoona hapa ni kutengeneza chuki kati ya CCM na wanajamii.

“Tunakwenda kwenye uchaguzi tukiwa na imani hiyo ila hakika 2020 kuna kazi kubwa, usione watu wamekaa kimya na hizi mbwembwe za chama, sisi wabunge wa CCM tunaamini wananchi si wajinga kwa kiwango ambacho tunawadhania.”

Mbunge mmoja wa viti maalumu wa chama hicho amesema kuwa, michezo ya kisiasa ni jambo la kawaida lakini uhai wa mtu ni jambo mtambuka.

“Tunapenda siasa na wengine haya ndio maisha yetu, lakini kuna jambo anaweza kutendewa mwenzako likakuumiza sana, hili la Lissu limeniumiza.

“Kuitendea nchi haki ni pamoja na kusimamia haki za kila mmoja licha ya kutofautiana naye mawazo. Tabia hujengwa na hii tabia ya kufungana midomo inajengwa,” amesema.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), tayari imetangaza uchaguzi kwenye jimbo hilo kwamba, utafanyika tarehe 31 mwezi huu ikiwa ni siku chache baada ya Spika Ndugai kueleza kuwa, jimbo hilo liko wazi.

Akitangaza uamuzi wa kumvua ubunge Lissu, Spika Ndugai alitaja sababu kuwa ni kutokana na mbunge huyo kuwa mtoro, pia kushindwa kujaza fomu ya maadili ya umma.

Kiongozi huyo wa Bunge alisema kuwa, amefuata utaratibu katika kumvua ubunge Lissu huku akiweza wazi kwamba, aliiandikia barua NEC kwamba, jimbo hilo lipo wazi.

Lissu alipigwa risasi zilizoelezwa kuwa 36 katika eneo la Area D muda mfupi baada ya kutoka bungeni tarehe 7 Septemba 2017, alikimbizwa Nairobi, Kenya kwa ajili ya matibabu na baadaye kupelekwa Ubelgiji kwa matibabu zaidi ambapo yupo mpaka sasa.

Wananchi na viongozi wa serikali wamekuwa wakimtembelea wakati akipatiwa matibabu. Miongoni mwao ni Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais ambaye alimtembelea Nairobi pia Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji alimtembelea.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

error: Content is protected !!