Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Michezo Sakata la kufungiwa Rais CAF, lawaibua TFF
Michezo

Sakata la kufungiwa Rais CAF, lawaibua TFF

Walace Karia, Rais wa TFF
Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa ufafanuzi juu ya kiasi cha dola za kimarekani 20, 000 (zaidi ya Tsh 43 milioni), zilizotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kwenda kwa Wallace Karia, ambaye ni Rais wa TFF. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

TFF imeeleza katika taarifa yake kuwa pesa hizo zinazodaiwa kuwekwa katika akaunti binafsi ya Rais wa TFF, Karia, hazikuwekwa kwenye akaunti binafsi.

Jana tarehe 23 Novemba, 2020 Shirikisho la Mpira wa Miguu Dunia (FIFA) lilimfungia kwa kipindi cha miaka mitano kutojihusisha na soka Rais wa CAF, Ahmad Ahmad kwa sababu za matumizi mabaya ya ofisi na fedha ikiwemo kutoa kiasi cha dola za kimarekani 20,000 kwenda kwa TFF na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Cap verde.

Katika taarifa yao TFF imeleeza kuwa Mei 2017, kamati tendaji ya CAF ilipitisha azimio ya kutoa kiasi cha dola za kimarekani 100,000  (zaidi ya Sh 231 milioni) kwa wanachama wake wote ambazo dola 80,000 (zaidi ya Sh 185 milioni) kwa ajili ya maendeleo ya soka na dola 20,000 kwa ajili ya Rais wa shirikisho husika kwa matumizi ya kila siku katika shughuli zao kwa kuwa hawalipwi mshahara.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf), Ahmad Ahmad

Taarifa hiyo iliendelea kwa kueleza kuwa mara baada ya fedha hizo kuingia kwenye akaunti ya TFF, Rais Kalia alitoa maelekezo kuwa kiasi hicho cha dola 20, 000 kitumike katika shughuli mbalimbali ndani ya shirikisho hilo kwa kuwa kulikuwa na uwaba wa fedha.

Hii ni mara ya pili kuibuka kwa sakata hilo la matumizi hayo ya fedha kwa TFF na kulitolea ufafanuzi mara kwa mara licha ya safari hii kuiba mara baada ya kuhusishwa na kufungiwa kwa Ahmad Ahmad, licha ya TFF kueleza kuwa kamati ya maadili ya FIFA kutozungumzia chochote kuhusu fedha hizo dola 20, 000.

Mara baada ya kufungiwa kwa Ahmad Ahmad, muda mchache CAF ilmtangaza Omar Selemani ambaye ni mujumbe wa baraza kuu la FIFA kuwa Rais wa muda wa shirikisho hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!