Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari Sakata la kina Mdee: Lissu ampinga Spika Tulia “ni uamuzi wa kisiasa”
HabariHabari za SiasaTangulizi

Sakata la kina Mdee: Lissu ampinga Spika Tulia “ni uamuzi wa kisiasa”

Spread the love

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)-Bara nchini Tanzania, Tundu Lissu ameukosoa vikali uamuzi wa Spika Tulia Ackson kuwabakisha bungeni Halima Mdee na wenzake 18. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Lissu amesema hayo muda mfupi kupita leo Jumatatu, tarehe 16 Mei 2022 tangu Spika Tulia kutoa uamuzi bungeni jijini Dodoma kwamba, hawezi kuwaondoa bungeni kwani wamefungua kesi mahakama.

Mdee na wenzake walifukuzwa Chadema 27 Novemba mwaka juzi na kamati kuu ya chama hicho wakituhumiwa kughushi nyaraka za chama, usaliti na kisha kujipeleka bungeni jijini Dodoma kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum.

Baada ya kufukuzwa, walikata rufaa Baraza Kuu la chama hicho lililokutana Jumatano hii jijini Dar es Salaam ambapo baada ya kuzisikiliza wajumbe 413 kati ya 423 zilikubaliana na kilichofanywa na kamati kuu ya kuwafukuza.

Spika Tulia amesema, anasubiri suala hilo la Mdee na wenzake waliokwenda mahakamani limalizike.

Hata hivyo, Lissu anayeishi nchini Ubelgiji ametoa andika kuhusu suala hilo ambapo linasomeka; Mbunge anapopoteza sifa ya kuwa mbunge, whether kwa kufukuzwa uanachama au kwa sababu nyingine yoyote, hastahili kuendelea kuwa mbunge kwa siku moja zaidi.

Na hali hiyo inaendelea hadi hapo Mahakama Kuu, au Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, itakapoamua vinginevyo.

Mimi nilivuliwa ubunge na Spika Ndugai. Nilikwenda Mahakama Kuu kuomba ruhusa ya kupinga uamuzi wa Spika mahakamani.

Niliponyimwa ruhusa hiyo nilikata rufaa katika Mahakama ya Rufaa. Rufaa hiyo haikusikilizwa hadi Bunge la 11 linakwisha muda wake.

The fact kwamba nilikuwa na rufaa mahakamani haikubadilisha status yangu ya kutokuwa na sifa ya kuendelea kuwa mbunge.

Mheshimiwa Lema alivuliwa ubunge na Mahakama Kuu. Alitolewa nje ya Bunge kwa kukosa sifa kutokana na kuvuliwa ubunge. Alikata rufaa Mahakama ya Rufaa, lakini aliendelea kuwa nje ya Bunge hadi Mahakama ya Rufaa ilioamua kwamba alikuwa mbunge halali.

Wabunge tisa wa chama cha CUF walifukuzwa uanachama wa kilichokuwa chama chao. Walitolewa Bungeni kwa kukosa sifa ya kuendelea kuwa wabunge.

Wabunge hao walifungua kesi Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa kuwafukuza uanachama. Kufungua kesi peke yake hakukuwarudisha Bungeni.

Mifano ya aina hii ni mingi sana katika historia yetu ya kisiasa na kibunge.

Spika Tulia Ackson anasemekana kuwa na PhD ya sheria. Alikuwa mwalimu wa sheria Chuo Kikuu na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Anajua sheria za nchi yetu na misingi yake. Uamuzi wake ni wa kisiasa; kwa sababu za kisiasa.

Ni wazi kwamba suala la COVID-19 ni suala la mfumo mzima wa utawala. Ikulu ya Magufuli ilihusika katika kuwaingiza Bungeni, na sasa Ikulu ya Samia inahusika na kuendelea kwao kuwa Bungeni.

Kwa Katiba na sheria zetu kama zilivyo sasa, Rais ndiye anayeamua malipo ya mishahara na posho za wabunge. COVID-19 wako Bungeni na wataendelea kuwa Bungeni sio kwa sababu wana kesi mahakamani, bali kwa sababu Samia anawalipa posho na mishahara yao.

Tuelekeze nguvu na mashambulizi yetu kunakostahili:

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!