July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sakata la CAG: Lema ampiku Mdee

Wabunge wa Upinzani wakitoka nje ya Bunge

Spread the love
MBUNGE wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, “amefukuzwa bungeni.” Amezuiwa kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Lema amekutwa na dhahama hiyo bungeni mjini Dodoma leo, tarehe A Aprili, kufuatia kauli yake aliyoitoa bungeni, kuwa Bunge la sasa, linaloongozwa na Job Ndugai, “ni dhaifu.”

Alitoa kauli hiyo, wakati wa mjadala uliotokana na kauli ya Halima Mdee, Mbunge wa Kawe (Chadema). Mdee alifikishwa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kwa madai kuwa amelidhalilisha Bunge. Amehukumiwa kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge.

Mdee alifikishwa mbele ya Kamati hiyo, kufuatia hatua yake ya kumuunga mkono, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad, aliyenukuliwa akisema, “Bunge ni dhaifu.”

Akiwasilisha ripoti yake bungeni, mwenyekiti wa kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka, alisema kuwa tarehe 2 Aprili mwaka huu, mbunge huyo wa Arusha Mjini, amelidharau na kulidhalilisha Bunge kufuatia matamshi yake, kuwa “Bunge ni dhaifu.”

Alisema, kufuatia matamshi hayo, kamati yake imependekeza kuwa Lema, aadhibiwe kwa kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo ya Bunge.

Mwakasaka alisema, “kufuatia kauli hiyo, mamlaka ya kiti yaliyowekwa kwa mujibu wa Kanuni 74 (1a & b) na Kanuni ya Nne (1 a & b), ilielekezwa kuwa mheshimiwa Lema, afike mbele ya Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge ili kuhojiwa kuhusiana na tuhuma hizo.

“Mheshimia Lema aliitikia wito wa kufika mbele ya Kamati. Lakini aliomba aruhusiwe kumleta wakili wake. Kamati ilitafakari na kuona kuwa Lema ni mbunge mzoefu wa vipindi viwili na pia aliwahi kuhojiwa na kamati hii; anajua kuhusu haki ya kuambatana na wakili wake, lakini hakuja naye. Kamati ilijadili na kuona kuwa Lema hakupanga kuja na wakili.”

Mwakasaka amesema, kwenye mahojiano yake mbele ya Kamati, Lema alikiri kuunga mkono maoni yaliyotolewa na Prof. Asad pamoja na Mdee.

Hivyo, kamati iliona naye ametenda kosa kwa mujibu wa kifungu cha 26(E) cha Sharia ya Haki. Akaomba Bunge kuidhinisha hukumu ya kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge.

Kufuatia hatua hiyo, baadhi ya wabunge wa wapinzani walilalamika kuwa kinachofanywa na Bunge ni kufuata utaratibu tu na siyo kushindana kwa hoja; kinachofikishwa mbele ya wabunge kinakuwa tayari kimeamuliwa na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kwa mujibu wa upinzani, Kamati ya Maadili ambayo inaundwa na wabunge wengi wa CCM na watatu kutoka upinzani, ndiyo inayowasilisha mapendekezo ya chama hicho bungeni na kupitishwa bila kujali hoja na taratibu.

Mara bvaada ya azimio la kumfukuza Lema bungeni kupitishwa, wabunge wote wa Chadema na baadhi ya kutoka Chama cha Wananchi (CUF), waliamua kutoka nje ya Bunge, kulalamikia walichokiita, “ubabe wa Spika, Job Ndugai.”

Lema amefikishwa mbele ya Kamati ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, kufuatia Naibu Spika, Dk. Tulia Akson Mwansasu, kuagiza kuhojiwa kufuatia kauli yake bungeni kuwa Bunge ni dhaifu. Dk. Tulia alisema, “kauli ya Lema, imelenga kulidhalilisha Bunge.”

Alisema, “…mnamjadili Mheshimiwa Mdee kwa kusema, Bunge ni dhaifu? Mimi kama mbunge wa vipindi viwili mfululizo, naweza kuthibitisha pasipo na shaka, kuwa Bunge hili, ni dhaifu mno.”

Sakata la Lema, lilianzia na hatua ya Spika Ndugai kuagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu huyo wa hesabu za Serikali, kwa madai ya kulidhalilisha Bunge.

Kilichomponza mtendaji huyo, ni kauli yake aliyoitoa katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya Umoja wa Mataifa nchini Marekani mwaka jana. nchini Marekani ambako alisema, “Bunge ni dhaifu.”

error: Content is protected !!