April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sakata la CAG bungeni; Mnyika, Chenge, Mhagama hapatoshi 

Spread the love

HATUA ya karatasi yenye orodha ya shughuli za Bunge (order paper) kutoonesha kuwepo kwa taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeibua mjadala. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Aliyeibua mjadala huo ni John Mnyika, Mbunge wa Kibamba jijini Dar es Salaam ambaye leo tarehe 9 Aprili 2019, aliomba mwongozo kwa Endrew Chenge, Mwenyekiti wa Bungena kuhoji sababu za kutokuwepo kwa ripoti ya CAG kwenye shughuli Bunge.

“Mapema leo asubuhi tumekabidhiwa orodha ya shughuli za leo ambayo pamoja na mambo mengine, kulikuwa na hati ya kuwasilisha mezani.

“Lakini Mheshimiwa Mwenyekiti, katiba ya nchi ibara ya 143 ibara ndogo ya 4 inasema, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali atawasilisha kwa rais kila taarifa itakayotoa kwa mujibu wa masharti ya ibara dogo ya pili,” amesema Mnyika wakati akitoa mwongoz wake na kuongeza:

“Baada ya kupokea taarfa hiyo, rais atawaagiza watu wanaohusika wakaiwasilisha taarifa hiyo kwenye kikao cha kwanza cha bunge kitakachofanyika baada ya rais kupokea taarifa hiyo, na itabidi iwasilishwe katika kikao hicho kabla haijapita siku saba tangu siku iliyoanza kikao hicho.”

Mbunge huyo amefafanua kuwa, iwapo rais hatowasilisha taarifa hiyo kwa mujibu wa Katiba ya Nchi ndani ya siku saba, CAG atawasilisha taarifa hiyo kwa Spika wa Bunge moja kwa moja.

“Endapo rais hatochukua hatua ya kuwasilisha taarifa hiyo kwenye bunge, basi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu atawasilisha taarifa hiyo kwa spika wa bunge au naibu spika.

“Ikiwa kiti cha spika kiko wazi au ikiwa kwa sababu zozote spika hawezi kutekeleza shughuli zake, basi ataiwasilisha taarifa hiyo kwenye Bunge.”

Akitete ahoja yake Mnyika ameliambia Bunge kwamba, taarifa ya CAG inaeleza kuwa tarehe 28 Machi 28 mwaka huu, rais alipokea ripoti za ukaguzi kutoka kwa Mwaka wa Fedha unaoishia June 2018.

“Na kikao cha kwanza cha bunge kilianza tarehe 2 ya mwezi huu, taarifa alizopokea rais hazijawasilishwa na Katiba imezungumzia siku saba, haijazungumzia siku za kazi au zisizokuwa za kazi.

“Naomba muongozo wako, ni kwanini katika orodha ya shughuli za leo hakuna ripoti ya CAG kwenye hati zilizowasilishwamezani?,” amehoji.

Mnyika amelitaka Bunge lieleze, ni lini rais ataagiza wanaohusika wawasilishe ripoti ya CAG bungeni kabla hazijapita siku saba.

Jenister Mhagama, Mnadhimu Mkuu wa Bunge kwa upande wa serikali aliomba mwongozi dhidi ya Mnyika.

Mhagama akimjibu Mnyika amesema, kwa mujibu wa utaratibu wa shughuli za bunge katika mijadala inayoendelea bungeni leo, aliyetangulia kuomba mwongozo ambaye ni Mnyika, ameonesha kutaka kujua tafsiri ya Katiba.

“Amejuka na kunukuu vifungu vya sheria ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, lakini hakwenda mbali zaidi.

“Hakusom sheria zingine zinazoambatana na maagizo hayo ya kikatiba na sheria katika kufanya tafsiri za siku, ambazo zimeandikwa kwenye Katiba na sheria husika na uwasilishaji wa ripoti ya CAG na hasa sheria ya tafsiri ya sheria,” amesema Mhagama.

Akisikilizwa kwa makini Mhagama amesema, Amelenga kuonesha wazi kwamba, serikali haitaki kuwajibika.

“Mheshimiwa mwenyekiti naomba muongozo wako, linapotokea jambo kama hili, kiti chako kipo tayari kumtafsiria Mnyika, tasfiri ya sheria hizo zote ili asiendeleee kulipotosha bunge na akatuacha serikali tuendelee kujipanga kwa kuzingatia sheria na taratibu husika katika utekelezaji wa jambo hili” Mhagama amesema.

Endrew Chenge, Mwenyekiti wa Bunge akijibu miongozo hiyo amesema kuwa, Katiba lazima isomwe sambamba na sheria zingine.

“Katiba kama ulivyoisoma lazima uisome na sheria nyingine, na sheria moja inayotuongoza ni sheria ya tasfiri za maneno yote ambayo yametumika kwenye sheria, sura namba moja ndio inayotumika.

“Kwa hiyo, kwanza suala lenyewe halikutokea bungeni, hakuna kitu kama hicho, nakusihi sana uende ukasome sheria ya tafsiri inapoeleza siku. Serikali haijaenda nje ya utaratibu unaotakiwa kwa mujibu wa Katiba” amesema Chenge.

error: Content is protected !!