March 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sakata la ‘Bashite’ kutolewa maelezo kesho

Boniface Jacob, Meya wa Manispaa ya Ubungo

Spread the love

TUME  ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inatarajia kumhoji Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob kuhusu  madai yake aliyowasilisha kwa tume hiyo akitaka Mkuu wa  Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwamba ameghushi vyeti vya shule, anaandika Faki Sosi.

Jacob amesema kuwa tume hiyo imemtaka afike ofisini kwao kesho asubuhi ili aweze kutoa maelezo juu ya mashtaka yake juu ya Makonda.

Meya huyo ambaye pia ni Diwani wa Ubungo amesema ameitwa kupitia barua yenye kumbukumbu namba  CAG 31/37/01/42.

Hata hivyo, Jacob amesema kuwa tayari kuna viashiria vya vishawishi vya yeye kuachana na shauri hilo linalomkabili Makonda.

Mwezi Machi mwaka huu  Jacob aliwasilisha mashtaka manne katika tume hiyo pamoja na moja la  jinai ambalo ni la kughushi  vyeti vya taaluma.

Hivi karibuni Makonda alipachikwa jina la Bashite ambalo linadaiwa ndilo jina lake halisi alilopewa na wazazi wake.

error: Content is protected !!