Sunday , 2 April 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Sakata la Balozi wa EU latinga bungeni, Spika aligomea
Habari za SiasaTangulizi

Sakata la Balozi wa EU latinga bungeni, Spika aligomea

Spread the love

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amegoma kuruhusu swali la Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe kutolewa majibu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, swali hilo lilihusu sakata la Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), Roeland Van de Geer kuitwa kwao. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Hivi karibuni Balozi, Van de Geer aliitwa makao makuu ya EU yaliyoko mjini Brussels nchini Ubelgiji kwa kile kilichoelezwa kuwa, kwenda kujadili masuala ya kisiasa na uhusiano baina ya Tanzania na jumuiya hiyo.

Wakati akiuliza swali kwa Waziri Mkuu, leo tarehe 8 Novemba 2018 bungeni jijini Dodoma, Mwambe alitaka kujua msimamo wa serikali kuhusu madai ya kudorola kwa mahusiano mazuri baina ya Tanzania na EU kufuatia hatua ya jumuiya hiyo kumuondoa balozi wake..

Lakini, Spika Ndugai alimzuia Waziri Mkuu kujibu swali hilo, akieleza kuwa maelezo ya swali hilo yanampa tabu kuruhusu swali hilo.

“Napata tabu kuruhu ili swali, maelezo yako unasema aliitwa huko kwao, sasa unataka waziri Mkuu ajibu nini?

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia apangua mawaziri

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la...

Habari za Siasa

RC mstaafu afariki dunia, CCM yamlilia

Spread the loveALIYEWAHI kuwa mkuu wa mikoa ya Dodoma, Mara, Mtwara na...

Habari za Siasa

Marekani kuwekeza Dola 500 Mil kupeleka bidhaa na huduma Tanzania

Spread the loveMAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amesema miongoni mwa...

Habari za Siasa

Kamala ataja hatua mpya kuimarisha uhusiano wa kibiashara Tanzania, Marekani

Spread the loveKATIKA kuimaridha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi baina ya Tanzania...

error: Content is protected !!