Thursday , 7 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Sakata la Babu Seya: Tujikumbushe matusi ya CCM
Habari za Siasa

Sakata la Babu Seya: Tujikumbushe matusi ya CCM

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jana tarehe 29 Agosti 2015, kimezindua kampeni zake katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.

Katika uzinduzi huo viongozi kadhaa wa chama hicho walihudhuria, wakiwemo Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Ufisadi, Edward Lowassa pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrance Masha ambao walihutubia mkutano huo wa ufunguzi.

Ni jambo la kushangaza kumsikia mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CHADEMA, Edward Lowassa, akihemewa na kujikuta akishindwa kuikabili hadhira ya Watanzania wanaofikia milioni 45 kuwaelezea ana malengo gani ya urais, chama chake kina dira na sera zipi za msingi, pia akizungumza bila kuonyesha mtiririko wa sera kupitia ilani ya uchaguzi ya chama hicho.

Mgombea wa CHADEMA, Bw. Lowassa ni dhahiri ameshindwa uchaguzi mkuu mapema, amebakia akilalama, kupiga soga na kujenga matumaini hewa kwa Watanzania huku akishindwa kujua ni changamoto zipi za msingi zinazowakabili wananchi katika maisha ya kila siku.

Lowassa akiwa anatetemeka jukwaani na kuongea kwa taabu amelizungumzia suala ambalo tayari “mahakama ya rufaa imekwisha litolea hukumu. Suala hilo ni kesi ya mwanamuziki Nguza Vicking na mwanawe Johnson Nguza waliohukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya ubakaji.”

Mahakama imedhibitisha kuwa Nguza Vicking maarufu kama “Babu Seya” na mwanaye Johnson Nguza maarufu kama “Papii Kocha” ni WABAKAJI, WANAJISI na WALAWITI. Na hivyo wamehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kutokana na tabia hizo chafu katika jamii.

Lowassa anakuja na hadithi ya kuwaachia huru, kana kwamba anaona vyombo vya sheria vimewaonea na kuwakandamiza.

Ifahamike kati ya makosa ambayo yameainishwa katika sheria za Tanzania, kosa la ubakaji halina msamaha. Mbakaji hawezi kupewa msamaha wa Rais. Msaidieni Lowassa maana anaonekana haijui sheria.

Tangu nchi imepata uhuru, hakuna Rais aliyewahi kutoa msamaha kwa wabakaji, wala walawiti. Lowassa anaonekana kuchanganyikiwa.

Ni dhahiri kwamba CHADEMA na mgombea wao Lowassa hawajajipanga kuongoza nchi. Hawana hoja za kuwasaidia watanzania, badala yake wanategemea siasa za matukio ili kujipatia kura. Tunaomba watanzania muwapuuze.

Imetolewa na:
Shaka Hamdu Shaka,
Kaimu Katibu Mkuu – UVCCM Taifa na Mjumbe wa NEC.

Hii ilikuwa taarifa iliyotolewa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kwa vyombo vya habari, tarehe 30 Agosti 2015.

1 Comment

  • Na Chadema watoe tena ile orodha yao ya mafisadi 11 waliyoitangaza pale Jangwani. Je bado wanawalaani hawa mafisadi 11 au wamegeuza nia?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

error: Content is protected !!