April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sakata la ATCL: Ubalozi wa Afrika Kusini – Tanzania ‘wavamia’

Spread the love

KUNDI la watu wachache limejitokeza leo tarehe 28 Agosti 2019, kwenye ofisi za ubalozi wa Afrika Kusini, uliopo kwenye barabara wa Shabani Robert jijini Dar es Salaam, wakishinikiza mahakama ya nchi hiyo iache huru ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL). Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Watu hao waliofika kwenye ubalozi huo asubuhi, bila kumtaja kiongozi wao, wamefika kwenye ubalozi huo wakiwa na mabango wakiimba ‘tunataka ndege yetu’.

Hata hivyo, polisi walifika eneo la tukio na kuwatawanya watu hao kwa maeleza kuwa, wamefanya mkusanyika na maandamano isivyo halali.

Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam amesema, watu wawili wamekamatwa kwa tuhuma za kuratibu maandamano hayo.

Taarifa ya kukamatwa ndege hiyonchini Afrika Kusini, ilitolewa na Dk. Leonard Chamuriho, katibu mkuu wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano tarehe 23 Agosti 2019.

Hata hivyo, Dk. Chamuriho hakueleza sababu ya kushikiliwa kwa ndege hiyo.

Baadaye msemaji wa serikali, Dk. Hassan Abbas kwenye taarifa yake alieleza kuwa, mkulima mmoja ambaye ni mdeni wake alipata amri ya mahakama kuu ya Gauteng, jijini Jonesburg kuzuia ndege hiyo kuondoka.

error: Content is protected !!