Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Tangulizi Sakata la ATCL: Serikali, Musiba waungana
Tangulizi

Sakata la ATCL: Serikali, Musiba waungana

Dk. Hassan Abbas, Katibu Mkuu wizara ya Habari
Spread the love

SIKU chache kupita baada ya Cyrispian Musiba, anayejitambulisha kuwa mtetezi wa Rais John Magufuli kudai, kukamatwa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) nchini Afrika Kusini ni hujuma, serikali nayo imetoa kauli ile ile. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Akizungumza na vyombo vya habari leo tarehe 31 Agosti 2019, Dk. Hassan Abbas, msemaji wa serikali amesema, sakata hilo limegubikwa na hujuma kutoka kwa baadhi ya Watanzania ambao hakutaja majina yao.

Pia, Dk. Abbas amesema, mgogoro huo wa sasa (wa kushikiliwa ndege hiyo) ukiisha, kila mmoja atabeba mzigo wake.

Kabla ya Dk. Abbas, Musiba ambaye ni mmiliki wa baadhi ya vyombo vya habari nchini alieleza kuwa, wanasheria, mawakili na wanasiasa wa Tanzania ndio walio nyuma ya sakata hilo kwa kumshawishi ‘mkulima’ kuibua sakata hilo.

Ndege hiyo aina ya Air Bus A220-300, ilishikiliwa nchini Afrika Kusini kwa amri ya Mahakama Kuu ya Gauteng, Johannesburg iliyotokana na kesi ya fidia iliyofunguliwa mahakamani hapo na Hermanus Steyn dhidi ya Serikali ya Tanzania.

Katika kesi hiyo, raia huyo wa Afrika Kusini ameeleza kuwa anaidai serikali ya Tanzania malipo yaliyobaki ya fidia ya mali zake zilizotaifishwa mwaka 1982.

Mbele ya wanahabari Dk. Abbasi ameeleza, kitendo cha Watanzania hao kushiriki kwa namna moja ama nyingine kufanikisha ukwamishaji huo, ni sawa na kuihujumu serikali, hivyo watafikishwa mahakamani kujieleza kwa nini walishiriki kosa hilo.

“Sasa ujumbe kwa hawa wanaofanya mawili matatu kuhangaika kutuhujumu, tuiache hii kesi iishe lakini mi nasema, kila mtu atabeba mzigo wake.

“Nchi hii ina sheria ukituhujumu ziko sheria za uhujumu uchumi zitatumika na usiseme haki za binadamu sababu umehujumu,” amesema Dk. Abbasi na kuongeza:

“Kwahiyo utakwenda mahakamani kwenda kueleza kwa nini umeihujumu nchi. Ukipatikana na hatia, utachukuliwa hatua. Kwa hiyo  siwezi kwa wakati huu kutaja majina ya watu lakini niseme hujuma zipo kwenye maeneo mbalimbali kama manabii walivyohujumiwa.”

Akizungumzia kesi hiyo, Dk. Abbasi amesema, wakati wowote kesi hiyo itatolewa uamuzi na anaamini kwamba ndege itaachiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme wang’oa vigogo TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewahamisha waliokuwa vigogo wa...

error: Content is protected !!