October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Safu mpya ACT-Wazalendo

Dorothy Semu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT wazalendo Bara

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimetangaza kuanza mchakato wa kupanga safu mpya ya uongozi wa chama hicho, kwa kufanya uchaguzi wake wa ndani. Anaripoti Martin Kamote, Dar es Salaam… (endelea).

Dorothy Semu, Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho amesema, pazia la uchukuaji na urejeshwaji fomu limefunguliwa leo tarehe 27 Januari 2020.

Amesema, nafasi zinazogombewa ni kiongozi wa chama, naibu kingozi wa chama, Mwenyekiti wa Taifa, Makamu Mwenyekiti Taifa-Tanzania Bara, Makamu Mwenyekiti Taifa-Zanzibar, Katibu Mkuu, Wajumbe wa Halimashauri Kuu (nafasi 15), Wajumbe wa Kamati Kuu (nafasi nane).

Ngome ya wanawake, nafasi alizotangaza ni pamoja Mwenyekiti wa Ngome, Makamu Mwenyekiti wa Ngome, Katibu wa Ngome, Naibu Katibu wa Ngome, Wajumbe wa Halimashauri Kuu Taifa (nafasi tatu), Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa (nafasi 5).

Ngome ya Vijana Taifa; nafasi zilizotangazwa ni Mwenyekiti wa Ngome, Makamu Mwenyekiti Ngome -Tanzania Bara, Makamu Mwenyekiti Ngome-Zanzibar, Katibu wa Ngome, Naibu Katibu wa Ngome, Wajumbe wa Halimashauri kuu Taifa (nafasi tatu), Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa (nafasi tano).

Ngome ya Wazee Taifa; nafasi zilizotangazwa ni Mwenyekiti wa Ngome, Makamu Mwenyekiti Ngome – Tanzania Bara, Makamu Mwenyekiti Ngome – Zanzibar, Katibu wa Ngome, Naibu Katibu wa Ngome, Wajumbe wa Halimashauri Kuu Taifa Nafasi (nafasi tatu),Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa (nafasi tano).

Dorothy amesema, uchukuaji fomu na kurejesha unaanza leo tarehe 27 Januari 2020 hadi tarehe 26 Februari 2020. Tarehe 7 Machi 2020 uchaguzi wa Ngome ya Wazee, tarehe 8 Machi 2020 uchaguzi wa ngome ya vijana, tarehe 9 Machi 2020 uchaguzi wa Ngome ya Wanawake, tarehe 14 Machi uchaguzi wa viongozi wakuu wa chama.

Amesema, fomu hizo zinapatikana katika Ofisi ya Makao Makuu Kijitonyama, Dar es Salaam; Ofisi Kuu, Vuga visiwani Zanzibar na ofisi za mikoa yote ACT Wazalendo.

error: Content is protected !!