Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Tangulizi Safu Mount Meru kufumuliwa
Tangulizi

Safu Mount Meru kufumuliwa

Dk. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Spread the love

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Godwin Mollel, ameagiza kuondolewa kwa safu ya uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru ikiwa ni sehemu ya maboresho katika sekta ya afya. Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Dk. Mollel ametoa agizo hilo wakati alipofanya ziara katika hospitali hiyo, na kuzungumza na timu ya uendeshaji wa huduma za Afya ya Mkoa ukiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dk. Wedson Sichalwe katika ofisi za Mganga Mkuu wa Mkoa huyo.

“Tumeona kwamba, Hospitali ya Mount Meru inahitaji mabadiliko makubwa sana ya kiuongozi, kwa kushirikiana na mamlaka husika, yafanyike haraka sana, kwasababu kuna mambo ya msingi sana yanayogusa Jamii ambayo yanatakiwa kufanywa kwa ustadi wa hali ya juu.” amesema Dk. Mollel.

Ameeleza kuwa serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwenye Sekta ya Afya, katika kuboresha miundombinu na huduma za afya zinazotolewa ili kuwasaidia wananchi wa vipato vya chini kupata huduma bora na nafuu bila wasi wasi.

“Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi sana kwenye eneo la Afya, Serikali imekuwa ikileta miundombinu mingi sana kwenye eneo la Afya, fedha ambazo Serikali imezileta kwenye eneo la afya zinatakiwa matokeo hizo fedha yamguse mwananchi wa kawaida,” amesema.

Ameongeza kuwa fedha zinazotolewa na Serikali kwaajili ya maboresho ya huduma za afya na miundombinu hazimgusi mwananchi wa kipato cha chini, ni lazima Serikali itafanya mabadiliko ili kuboresha Sekta hiyo kutoa huduma bora na nafuu kwa wananchi.

Nae Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dk. Wedson Sichalwe amesema Serikali imeboresha miundombinu katika Sekta ya Afya na utoaji huduma ikiwemo hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, ili kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini kupata huduma bora na nafuu.

“Mpaka sasa kazi ambayo imefanywa na Serikali ya kuboresha miundombinu ya Sekta ya Afya, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, katika vituo vyetu imeboreshwa, miongozo ipo, kwahiyo shida kubwa ipo katika usimamizi na ndio eneo kubwa ambalo tumeagizwa,” amesema.

Dk. Wedson amepokea agizo la usimamizi mzuri wa Sekta ya Afya katika Mkoa wa Arusha na Halmashauri zake lililotolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Mbali na hayo, Dk. Wedson amesema kuwa, imeendelea kutoa elimu ya mafunzo kwa wanaojihusisha na masuala ya utalii 360, lengo ni kuhakikisha kuwa wanawapokea vizuri Watalii na kuweza kuchukua hatua zinazostahili pindi shida yoyote inapojitokeza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!