Saturday , 10 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Safari za meli kutoka Tanzania-Msumbiji, Malawi yazinduliwa
Habari Mchanganyiko

Safari za meli kutoka Tanzania-Msumbiji, Malawi yazinduliwa

Kassim Majaliwa, akikagua meli ya MV Mbeya II
Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amezindua rasmi safari ya meli mpya ya MV Mbeya II itakayotoa huduma katika Ziwa Nyasa nchini na nchi jirani za Msumbuji na Malawi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Ruvuma … (endelea).

Meli hiyo yenye thamani ya Sh.9.1 bilioni ni muendelezo wa Serikali ya awamu ya tano wa kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji wa mizigo na abiria kwa lengo la kuboresha uchumi.

Amezindua  safari za Meli hiyo jana Jumanne, tarehe 5 Januari 2021 katika Bandari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa.

Amewataka wananchi waitunze meli hiyo ambayo imejengwa na kampuni ya Kitanzania ya Songoro Marine.

Waziri mkuu amesema, Tanzania imezungukwa na nchi nane ambazo zinategemea kupata bidhaa mbalimbali kutoka nchini.

“Wananchi tumieni fursa ya uwepo wa meli hii kufanya biashara,” amesema Majaliwa.

Amesema wananchi hawawezi kupata maendeleo bila ya Serikali kujenga miundombinu kama ya meli, barabara, bandari, hivyo amewataka waitumie vizuri kwa ajili ya kukuza uchumi wao.

“Serikali inajenga vitu kwa maendeleo ya watu na kwa kuzingatia hilo, Serikali imewekeza fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu itakayowanufaisha kiuchumi kama meli.”

Kadhalika, Waziri Mkuu ameagiza kuwe na kanzidata ya mafundi chipukizi wa Kitanzania wanaoshiriki katika ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati kama meli na madaraja makubwa.

Majaliwa amesema, kanzidata hiyo itaiwezesha mafundi hao chipukizi kutambuliwa kwa lengo la kuwaendeleza zaidi na kuwa na ujuzi ili baadaye wapewe miradi ya ujenzi.

Pia, waziri mkuu alikagua hali ya ujenzi wa mradi wa barabara ya Mbinga-Mbambabay yenye urefu wa kilomita 66 ambayo ujenzi wake umekamili. Amesema ameridhishwa na ujenzi wake.

“Nimekuja na barabara hii nateleza tu, wakati ule ulikuwa unatembea katika mawe, makorongo lakini sasa unalala tu. Naipongeza kampuni ya CHICO kwa ujenzi wa mradi huu.”

Naye, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema, ujenzi wa barabara hiyo ni kutimiza ndoto za Rais John Pombe Magufuli za kuboresha miundombinu.

Amesema kukamilika kwa barabara hiyo pamoja na kuanza kwa safari ya meli  ni ukombozi wa kiuchumi kwa wananchi wa wilaya ya Nyasa na ukanda mzima wa kusini. “Sasa Nyasa imefunguka.”

Mhandisi Kasekenya amesema Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi itahakikisha inasimamia kikamilifu bandari katika kukusanya mapato yake kwa njia ya kielektroniki ili ziweze kujiendesha na kwamba haitamvumilia mtendaji yeyote atakayekwenda tofauti.

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara wa Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Alinanuswe Lazeck amesema ujenzi barabara ya Mbinga-Mbamba Bay yenye urefu wa kilomita 66 umegharimu Sh.129.361 bilioni.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Deusdedit Kakoko alisema katika ziwa nyasa kuna jumla ya bandari 15 kati yake sita zipo mkoani Ruvuma, sita zipo mkoani Njombe na tatu zipo mkoani Mbeya.

Alisema katika kuboresha usafiri katika Ziwa Nyasa Serikali ilitoa Sh.20.1 bilioni ambazo zimetumika katika kujenga meli tatu ambazo kati yake mbili ni za mizigo MV Ruvuma na MV Njombe kwa thamani ya Sh.11 bilioni na meli ya abiria na mizigo ya MV Mbeya ii kwa Sh.9.1 bilioni. Meli ya MV Mbeya ii inauwezo wa kubeba abiria 300 na tani 200 za mizigo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi zaidi ya 100 wapigwa msasa wa udereva kukabiliana na ajali

Spread the love  KATIKA kuhakikisha wimbi la ajali za barabarani zinapungua kama...

Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali yakana kuhamisha kwa nguvu jamii ya Kimasai Loliondo

Spread the loveWAZIRI wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro,...

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

error: Content is protected !!