July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Safari ya JK kung’oka uenyekiti CCM yaiva

Spread the love

SAFARI ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Jakaya Kikwete kuondoka kwenye nafasi hiyo imeiva, anaandika Dany Tibason.

Anayetarajiwa kushika nafasi hiyo ni Dk. John Magufuli ambaye ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tayari leo tarehe 3 Mei Kamati Kuu ya Halmashauri ya Taifa ya CCM imeanza kukutana katika Ikulu ya Chamwino na kupitisha majina ya wagombea kwenye nafasi mbalimbali.

Miongoni mwa nafasi hizo ni wabunge wa CCM wa Bunge la Tanzania 21 walioomba nafasi ya ujumbe wa halmashauri kuu ya taifa.

Christopher Ole Sendeka, Msemaji wa CCM akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano katika Jengo la CCM-Makao Makuu mjini Dodoma, amesema chama hicho kimeanza utaratibu wa kawaida wa kukabidhiana vijiti.

Amesema, kutokana na utamaduni ambao chama hicho umeuweka, Dk. Kikwete atakabinyi kijiti hicho kwa Rais Magufuli ili kuweza kukijenga chama hicho.

“Kwa utamaduni wa CCM ambao umekuwepo kuanzia kwa rais wa awamu ya pili kurithishana mafasi kabla ya kumalizika kwa miaka mitano, ndivyo hivyo ambavyo hata Jakaya na Magufuli watakavyo fanya.

“Kimsingi kama ingekuwa ni kufuata Katiba ya CCM, Kikwete alitakiwa kukabidhi nafasi hiyo mwaka 2017 kwa malengo ya kutimiza kipindi cha miaka mitano lakini kutokana na utamaduni wetu, wameishakubaliana kukabidhiana majukumu hayo na sasa mandalizi yanafanyika,” amesema Ole Sendeka.

Pia amesema, Kamati Kuu ya Halmashauri ya Taifa ya CCM iliyokutana leo katika Ikulu ya Chamwino, imepitisha majina ya wabunge wa CCM wa Bunge la Tanzania 21 walioomba nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.

Aliwataja wabunge hao waliopitishwa kuwa ni Munde Tambwe Abdallah, Jamali Kasssim Ali, Faid Mohamed Bakari, Mbaraka Kitwana Dau, Alex Laphael Gashaza.

Wengine ni  Hawa  Ghasi, Ibrahim Riza, Angellah Kairuki, Dk. Hamisi Kigwangwala , Livingstone Joseph Lusinde, Dk. Angeline Sylester Mabula, Almas Athuman Maige, Angelina Adam Malembeka, Agnes Mathew Marwa, Yahaya Omary Massare.

Wengine  ni Stephen Hirary Ngonyani, Stanslaus Nyongo, Mattar Ali Salum, Peter Serukamba na Hafidh Ali Tahir.
Ole Sendeka amesema, Halmshauri Kuu imepitisha majina 19 ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walioomba kugombea nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kupitia Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Ametaja waliopitishwa kuwa ni Nassor Salim Ali, Ali Khamis Bakari, Mgeni Hassan Juma, Riziki Pemba Juma, Yussuf Hassan Iddi, Khadija Omar Kibano, Shamata Shaaame Khamis, Mmanga M. Mjawiri.

Wengine ni Dk. Khalid Salum Mohamed, Asha Abdalla Mussa, Mihayo Juma N’hunga, Zulfa Mmaka omar, Hamad Abdalla Rashid, Mohamed Ahmada Salum, Harusi Said Suleiman, Haroun Ali Suleiman, Issa haji Ussi na Bahati Khamis  Kombo.
amesema Kamati Kuu pia imepitisha majina ya Wabunge wa CCM wanne, walioomba  nafasi ya  Katibu wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM.
ametaja majina hayo kuwa ni  Jason Samson Rweikiza, Mary Pius Chatanda,  Mariam Nassoro Kisangi na  Abdala Hamis Ulega.
Ole Sendeka amesema Halmashauri Kuu imepitisha majina matatu ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walioomba nafasi ya Katibu wa Kamati ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM.
Majina yao ni Abdallah Ali Kombo, Ali Suleiman Ali maarufu kwa jina la (Shihata) na Ali Salum Haji.

Katika kikao hicho pia Kamati Kuu imepitisha majina ya wanaCCM walioomba nafasi mbalimbali za uongozi.
Amewataja wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Wilaya ya Handeni kuwa ni Omar Abdallah Kigoda, Maajabu Athuman Hamis, Mussa Said Kidato, Hamis Hamad Mnondwa na Athuman Yahaya Lukoya.

Katibu wa Uchumi na Fedha, Mkoa wa Mbeya aliwataja kuwa ni Charles Michael Mwakipesile, James Mwampondele Mwasunga na Stephen Issac Mwakajumulo.

Katika Mkoa wa Njombe, Katibu wa Uchumi na Fedha ni  Creiton Patric Lulambo, Salu Batwel Sanga na Reuben Erick.

Amesema kwamba, kwa sasa wale wote ambao majina yao yamepitishwa wanaruhusiwa kufanya kampeini za kistaarabu na kwamba, atakayebaini kufanya makosa atachukuliwa hatua kali.

error: Content is protected !!