May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

SADC kupeleka jeshi Msumbiji

Spread the love

 

NCHI Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (​SADC), zimekubaliana kupeleka wanajeshi kukabiliana na ugaidi katika Jimbo la Cabo Delgado, Msumbiji. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Makubaliano hayo yalifikiwa katika mkutano wa marais wa jumuiya hiyo uliofanyika mjini Maputo, Msumbiji ili kujadili tatizo la ugaidi, maingiliano na manedeleo ya kikanda.

Marais na viongozi wa serikali wa nchi 16 wanachama wa jumuiya hiyo wameadhimisha miaka 40 tangu kuundwa kwa jumuiya hiyo.

Kwenye mkutano huo, marais hao walijikita kuhusu hali ya usalama kwenye Jimbo la Cabo Delgado, Kaskazini mwa Msumbiji.

Katibu mtendaji wa jumuiya hiyo Stragomena Pax, amesema marais hao walikubalian kupeleka kikosi cha pamoja cha jumuiya hiyo nchini Msumbiji.

Faustin Luanga, Mshauri wa Maswala ya kimaitafa wa rais wa Congo, Felix Tshisekedi na ambaye ni mgombea wa wadhifa wa katibu mtendaji wa jumuiya hiyo, ameelezea ajenda ya mkutano huo.

”Mkutano ulianza toka Jumatatu ambapo wataalamu walikutana, wakifuatiwa jana na mawaziri ambao wameadhimisha miaka 40 ya kuundwa kwa Jumuiya ya SADC.

“Mkutano uliendelea vizuri, walizungumzia masuala ya siasa na hasa usalama huko Cabo Delgado Msumbiji,” alisema Luanga.