May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sabaya wenzake wanusa miaka 200 jela

Lengai ole Sabaya

Spread the love

 

MASHITAKA sita yanayomkabili Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro, nchini Tanzania, aliyesimamisha kazi, Lengai ole Sabaya, yaweza kumuweka kwenye kifungo cha miaka 200 gerezani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Sabaya anaweza kufungwa miaka 30 katika kila kosa katika makosa sita yanayomkabili yeye pamoja na wenzake watano.

Hata hivyo, endapo Sabaya na wenzake, watapatikana na hatia katika makosa yanayowakabili, wanaweza kutumikia kifungo cha miaka 30 gerezani, iwapo adhabu hiyo itakwenda kwa pamoja.

Wenzake ni; Enock Togolani Mnkeni (41), mkazi wa Arusha; Watson Stanley Mwahomange (27), mkazi wa Sakina, Arusha; John Odemba Aweyo, mkazi wa Arusha na Sylvester Wenceslaus Nyengu (26), mkazi wa Sokoni One, Arusha

Wakili anachambua kwa kina adhabu ambazo Sabaya na wenzake watakutana nazo kwenye mashtaka yanayowakabili kwa mahakimu wawili tofauti. Nafuu ipi wanaweza kuipata mahakamani. Zaidi soma Gazeti la Raia Mwema, la leo Jumatano, tarehe 9 Juni 2021.

error: Content is protected !!