May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sabaya, wenzake waachiwa huru

Spread the love

MAHAKAMA Kuu ya Kanda ya Arusha imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili waliokuwa wamekata rufaa ya kupinga kuhukumiwa miaka 30 kwenda jela kila mmoja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea)

Mahakama imewaachia huru kwakuwa Mrufani namba mbili Silvester Nyegu na namba tatu Daniel Mbura hawakupewa haki ya kumhoji Shahidi namba mbili wa Jamhuri na kutokufanya hivyo kunawanyima haki yao msingi.

Jaji aliyekuwa akisikiliza rufaa hiyo, Ezedekia Kisanya amesema kulikuwa na mkanganyiko kwenye mwenendo wa usikilizwaji wa kesi hiyo ikiwemo kutofautiana kwa mashahidi na kuufanya ushahidi kuwa batili.

Jaji amesema watakuwa huru endapo watakuwa hawana kesi nyingine kwenye Mahakama yoyote.

error: Content is protected !!