Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Sabaya na wenzake wasomewa mashtaka 5, wakosa dhamana
Habari MchanganyikoTangulizi

Sabaya na wenzake wasomewa mashtaka 5, wakosa dhamana

Spread the love

 

LENGAI Ole Sabaya, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro na wenzake watano, wamesomewa mashtaka matano, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, ikiwemo unyang’anyi kwa kutumia silaha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Sabaya na wenzake watano, wamefikishwa katika mahakama hiyo leo Ijumaa, tarehe 4 Juni 2021, wakiwa katika gari ndogo ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Sabaya na wenzake watano ambao ni; Sylivesta Nyegu, Wadson Stanley, Enock Togolan, John Odemba na Daniel Mbura, wamesomewa mashtaka matano katika kesi mbili tofauti mahakamani hapo.

Mashtaka mengine ni; uhujumu uchumi, unyang’anyi kwa kutumia silaha, kushiriki vitendo vya rushwa alipokea Sh.90 milioni, kutakatisha fedha na kuongoza magenge ya uhalifu.

Kesi ya kwanza, imesikilizwa na Hakimu Martha Mahumbuga na ya pili yenye ya jumla ya mashtaka mawili ya unyang’anyi kwa kutumia silaha na kushambulia aliowanyang’anya imesikilizwa na hakimu mwingine.

Nje ya Mahakama, mkurugenzi msaidizi ofisi ya mashtaka, anayeshughulikia usimamizi wa kesi, Tumain Kweka amesema, uchunguzi kwa baadhi ya makosa, “yanayomkabili Lengai na wenzake, yamefikia tamati ya kuwafikisha mahakamani.”

“Baada ya DPP kujiridhisha, ameamua kuwafikisha mahakamani, alikuwa anatuhumiwa kuendesha magenge ya uhalifu, vitendo vya rushwa, kutakatisha fedha na unyany’anyi wa kutumia silaha,” amesema Kweka.

Amesema, unyany’anyi wa kutumia silaha ni makossa mawili aliyoyatenda kwa watu wawili tofauti.

Mashtaka hayo kwa mujibu wa sheria, hayana dhamana hivyo, Sabaya na wenzake wamepelekwa gerezani hadi tarehe 18 Juni 2021, itakapotajwa tena.

Sabaya amefikishwa mahakamani baada ya kushikiliwa kwa zaidi ya siku kumi na Takukuru, kwa maagizo ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Tarehe 13 Mei 2021, Rais Samia alimsimamisha kazi, Sabaya ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zilizokuwa zinamkabili.

1 Comment

  • Hewallah – Safi sana.- Mbona hamtoi na habari za Manji? – Kama anashikiliwa na Takukuru ni lini atafikishwa mahakamani ili tujue makosa yake ni nini?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!