ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Hai (DC), mkoani Kilimanjaro, Lengai ole Sabaya, yuko mafichoni, akitafakari hatma yake ya baadaye, Raia Mwema limeelezwa. Anaripoti Mwanandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Vyanzo vya taarifa kutoka kwa watu walioko karibu na Sabaya vinasema, mwanasiasa huyo amejichimbia katika hoteli moja, iliyopo maeneo ya Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.
Sabaya alisimamishwa kazi tarehe 13 Mei 2021 na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazimkabili.
Wakati Sabaya anatangazwa kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi, alikuwa mkoani Dodoma, akitokea jijini Dar es Salaam ambako alifanya mahojiano maalum na kituo kimoja cha televisheni.
“Huyu bwana yuko mafichoni pale Mbezi Beach, eneo la Afrikana, ambako amejichimbia kwa takribani wiki moja sasa,” ameeleza mtoa taarifa wa gazeti hili.
Undani wa kusimamishwa kwake, alikuwa wapi? Alirudi Hai au la, hotel aliyojificha, mabaunsa wake na mengine mengi, soma Gazeti Raia Mwema leo Jumamosi, tarehe 22 Mei 2021.
Leave a comment