Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sababu za kutemwa Mwijage, Tizeba hizi hapa
Habari za Siasa

Sababu za kutemwa Mwijage, Tizeba hizi hapa

Spread the love

RAIS John Magufuli ametaja sababu za kuwaondoa, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Charles Tizeba na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, akisema kuwa baadhi ya majukumu yao yalikuwa yakitekelezwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza baada ya kuwaapisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Josephat Kakunda na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, Rais Magufuli ametaja baadhi ya majukumu ambayo Mwijage na Tizeba walishindwa kuyatekeleza wakati wa uongozi wao, ikiwemo katika kutatua sakata la zao la korosho, kahawa na migogoro ya viwanda.

“Kwenye Sakata la kahawa, waziri mkuu alienda kule alienda kusolve ‘kutatua’, najiuliza kahawa ni kilimo kinalimwa, nikasema waziri wa kilimo hakujua kahawa ni zao, kiwanda cha chai cha Mbonde kimekaa miaka 8, wakulima chai yao imeharibikia kwenye mashamba tatizo halijashughulikiwa.

Nikamtuma waziri mkuu akaenda akalitatua nikamueleza nitakufanya uwe waziri wa kilimo au wa viwanda, mpaka ukaenda kusolve wewe, nikasema kwa nini hawa nilio wapa majukumu haya hawasolve hivi? Hiyo ni baadhi ya mifano.” Amesema.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amesema baadhi ya taasisi zilizo chini ya wizara hizo, zimeshindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo, ikiwemo kutafuta masoko na kupanga bei ya mazao ya wakulima.

Miongoni mwa taasisi hizo ni pamoja na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Bodi ya Mazao Mchanganyiko ambayo kazi yake ni kupanga bei za mazao, bodi za pamba, korosho na tumbaku.

“Kuna bodi ya mazao mchanganyiko iko pale tangu enzi za baba wa taifa jukumu lake ni kuregulate bei na kutafuta soko nje na kuuza mazao, kuna TANTRADE ambayo jukumu lake ni kutafuta biashara ya mazao hata madini, na bodi nyingine mbalimbali za mazao, bodi ya pamba, korosho, tumbaku zote zina wataalum wazuri sana, lakini linakofika suala la mazao ya watanzania hawashughuliki,

“Kwenye bajeti ya Malawi imetenga kiasi cha dola 27.2 milioni fedha za kununua vyakula, bodi hizi zimefanya jitihada gani kwenda kutafuta soko, unapoona kuna kilio kikubwa waziri mkuu anaenda kutatuta, ninampenda sana Mwijage nampenda sana Tizeba lakini kwa hili hapana.” Amesema Rais Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!