August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Saanya, Mpenzu waondolewa Ligi Kuu

Wachezaji wa Simba wakimzonga mwamuzi wa mchezo wao dhidi ya Yanga, Martine Saanya (kushoto)

Spread the love

WAAMUZI waliochezesha mchezo namba 49 kati ya Yanga na Simba katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Martin Saanya na Samwel Mpenzu wametolewa katika ratiba ya michezo ya ligi hiyo huku suala lao likipelekwa kwenye kamati ya waamuzi ili lishughulikiwe kitaalamu.

Maamuzi hayo yamefanyika baada ya kamati ya usimamizi na uendeshaji ya bodi ya ligi kuwaita na kuwahoji na kuangalia mkanda wa mchezo husika na kamati kubaini mapungufu mengi ya kiutendaji yaliyofanywa na waamuzi hao na hivyo kutaka kamati ya waamuzi iwashughulikie.

Saanya na wenzake walichezesha huo Oktoba Mosi mwaka huu na kumalizika kwa sare ya bao 1-1, huku wakionekana kushindwa kumudu mchezo huo na kufanya maamuzi yaliyoleta utata mkubwa kama kukubali bao la mkono la Amis Tambwe na kadi nyekundu aliyotoa kwa Jonas mkude hali iliyopelekea uvunjifu wa amani na uvunjwaji wa viti uwanjani.

Pia mwamuzi Rajabu Mrope aliyechezesha mchezo kati ya Mbeya city na Yanga naye ametolewa kwenye ratiba ya ligi kuu katika mzunguko wa pili baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kutojiamini mchezoni pamoja na kukubali goli, kasha kukataa na mwisho kukubali tena na suara lake kurudishwa kwenye kamati ya waamuzi ili kumpangia daraja lingine la uwamuzi.

Katika ligi ya Daraja la kwanza, Mwamuzi Thomas Mkombozi aliyechezesha mechi namba 15B kati ya Coastal Union na KMC ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi kutokana na kushindwa kuudhibiti mchezo na kutoshirikiana na wasaidizi wake baada ya kamati kufanya mahojiano nao na kugundua mkombozi alifanya maamuzi mengi pasipo kuwa makini.

Lakini pia klabu ya Coast Union imepewa adhabu ya kucheza bila ya mashabiki kwa mechi mbili za nyumbani na mechi moja ya nyumbani kuchezwa uwanja wa ugenini kwa kosa la mashabiki wa timu hiyo kumshambulia Mwamuzi.

kuhusu Mwamuzi Ahmed Seif, Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji ya bodi ya Ligi, imemfungulia na kumtoa kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi kuu mwamuzi huyo aliechezesha mchezo namba 28 kati ya African Lyon na Mbao FC. hivyo, Mwamuzi Ahmed Seif atarudishwa kwenye kabati ya waamuzi ili apangiwe majukumu mengine.

error: Content is protected !!