Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Saa 72 za moto Chadema
Habari za SiasaTangulizi

Saa 72 za moto Chadema

Spread the love

CHAMA Kikuu cha Upinzani nchini Tanzania cha Chadema, kinaingia siku tatu ngumu za mchakato wa kupata mgombea urais wa Tanzania na Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Chadema kitaanza mikutano yake kesho Jumapili tarehe 2-4 Agosti, 2020 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Pia, Chadema kitatumia mikutano hiyo, kuwapata wagombea ubunge, wawakilishi na madiwani wa viti maalum na wabunge wa viti maalum.

         Soma zaidi:-

Kesho Jumapili, itakuwa ni kikao cha Kamati Kuu ya Chadema, Agosti 3, zamu ya Baraza Kuu na mwisho Agosti 4 itakuwa ni mkutano mkuu.

Awali, mikutano hiyo ilipangwa kufanyika kati ya tarehe 27 hadi 29 Julai 2020, lakini ikasogezwa mbele kutokana na msiba wa Hayati Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa.

Mkapa alifikwa na mauti Alhamisi tarehe 23 Julai 2020 saa 3:30 usiku katika moja ya hospitali jijini Dar es Salaam kwa mshituko wa moyo.

Mwili wa Mkapa, ulizikwa kijijini kwao, Lupaso wilayani Masasi Mkoa wa Mtwara tarehe 29 Julai.

Chadema, kinachoongozwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe kitatumia siku hizo tatu (sawa na saa 72) kumpata mgombea Urais wa Tanzania na Zanzibar.

Wanachama saba wanachuana kuwania kunyang’anyiro cha Urais wa Tanzania ambao ni; Wakili Simba Neo, Lazaro Nyalandu, Tundu Lissu, Wakili Gasper Mwanalyela, Isaya Mwita, Mchungaji Leonard Manyama na Dk. Myrose Majinge.

Waliojitokeza Zanzibar ni; Said Issa Mohamed, makamu mwenyekiti wa Chadema-Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Chadema, Hashim Issa Juma na Mohammed Ayoub Haji.

Nafasi kwa wagombea wa Tanzania, inatolewa kwa wanachama wawili ambao ni Lazaro Nyalandu na Tundu Lissu.

Nyalandu ambaye ni mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati aliyewahi kuwa waziri wa maliasili na utalii katika utawala wa awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amewatakia safari njema wajumbe wa mikutano hiyo ya Chadema.

Nyalandu ametumia ukurasa wake wa Twitter, kuwaeleza kwamba wanajua cha kufanya pasina kufuata maelekezo kutoka juu.

Mshindani wake, Lissu tayari amekwisha rejea nchini kutoka Ubelgiji alikokuwa kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi 30 na watu wasiojulikana mchana wa tarehe 7 Septemba 2017.

Lissu ambaye ni makamu mwenyekiti wa Chadema-Bara, alikutwa na mkasa huo akiwa ndani ya gari lake eneo la Area D jijini Dodoma alipokuwa akirejea kutoka bungeni.

Lissu na Nyalandu watachuana vikali ili kumpata mgombea urais atakayechuana na wagombea wa vyama vingine akiwemo Rais John Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

John Mrema, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, akizungumza na MwanaHALISI Online leo Jumamosi tarehe 1 Agosti 2020 amesema, maandalizi yanendelea vizuri.

“Maandalizi yanaendelea ya kuanza safari ya kumtafuta mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, makamu wa Rais, Rais wa Zanzibar, wagombea ubunge, uwakilishi na madiwani,” amesema Mrema.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Amesema, madiwani watakaohusika ni wa viti maalum lakini wale wa kugombea watakapotoka ngazi ya wilaya.

Mrema amesema, mikutano hiyo mitatu itapitisha Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Chadema.

Amesema, wamejipanga kuhakikisha wanapata mgombea anayekubalika bila kutumia rushwa au mashinikizo na atakayebainika kutumia njia zisizostahili, watamchukulia hatua.

Dk. Myrose Majinge, mgombea

Kuhusu kauli ya Nyalandu kuwatakia safari njema wajumbe na kuwaeleza wasisikilize maelekeso kutoka juu, Mrema amesema, “ni mbinu za medani za kitafuta kura na hizo ni sehemu za mbinu tu.”

“Vile vile wajumbe wa vikao vya Chadema, hawaji kwa maelekezo na wao wenyewe wanajua cha kufanya. Hizi kauli ni mbinu za kutafuta kura kwa mwingine anakwenda mitandaoni na mwingine anafanya kimya kimya,” amesema.

Mrema amesema, “uhakika, hakutakuwa na rushwa na wajumbe wetu hawakubaliana na rushwa na akijaribu kutoa rushwa atachinjwa. Tunawatakia kila la kheri wagombea wote.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

error: Content is protected !!