RAIS wa Tanzania, John Magufuli atafanya ziara ya kikazi ya siku tatu, jijini Dar es Salaam, kuanzia Jumatano hadi Ijumaa, tarehe 26 Februari 2021. Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).
Katika ziara hiyo ya siku tatu sawa na saa 72, Rais Magufuli atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyokwisha na inayoendelea.
Akizungumza kuhusu ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge amesema, ziara hiyo itaanza Jumatano tarehe 24 February 2021.
Amesema, siku hiyo saa 3:30 asubuhi, Rais Magufuli, atazindua Daraja la Juu Ubungo (Ubungo interchange) na mara baada ya hapo, atakwenda Mbezi kwaajili ya uzinduzi wa Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi cha Mbezi Luis, saa 05:30 asubuhi.
Aidha Kunenge amesema, Alhamis, Rais Magufuli, ataweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Soko la kisasa Kisutu, saa 03:30 asubuhi na baada ya hapo atafanya shughuli ya uzinduzi wa Jengo la Jitegemee House ambapo Kuna Studio za Channel ten na Uhuru Fm.
Kunenge amesema, siku ya Ijumaa, Rais Magufuli, atafanya shughuli ya uzinduzi wa majengo ya Chuo Cha Polisi na Kiwanda Cha kutengeneza sare za Polisi ambapo tukio hilo litafanyika saa 03:30 asubuhi.
Leave a comment