November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rwanda wadai kumuua mwanajeshi wa DRC

Spread the love

JESHI la Rwanda limedai kumuua mtu anayeaminiwa kuwa mwanajeshi kutoka nchi jirani ya DRC, katika Wilaya iliyopo mpakani ya Rubavu.

Tukio hilo limejiri huku uhusiano kati ya nchi hizo mbili ukizidi kutetereka kutokana na Congo kuituhumu Rwanda kuunga mkono waasi wa M23 wanaoitesa nchi hiyo. Anaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Ripoti iliyotolewa na jeshi la Rwanda inasema mtu huyo aliyekuwa amevalia magwanda ya jeshi la DRC na ambaye hakutambuliwa mara moja, anaamiwa kuwa mwanajeshi wa FARDC.

Aidha, jeshi la Rwanda linasema mtu huyo alivuka kizuizi cha “Petite Barrière” na kuanza kuwafyatulia risasi maafisa wa usalama, wakati alipopigwa risasi na mwanajeshi wa nchi yake kuepusha madhara zaidi.

Afisa wa DRC ambaye alikuwa katika eneo la tukio na kutotaka kufahamika amesema hakuna mwanajeshi wa DRC aliyekuwa anaweka doria katika eneo hilo la mpaka, licha ya makabiliano ya risasi kusikika usiku kucha.

Tukio hili limetokea baada ya mapema mwezi huu, ndege ya kivita ya DRC kuvuka mpaka wa anga bila ya idhini na kutua katika uwanja wa ndege wa Rubavu na kuikasirisha Rwanda.

error: Content is protected !!