July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rwamlaza ataka shule zihamishwe

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum, Conchesta Rwamlaza (Chadema), amehoji Serikali  ina mpango gani wa kuzihamisha shule za msingi Tumaini na Zamzam katika Manispaa ya Bukoba, ambazo zipo karibu na uwanja wa ndege hasa baada ya upanuzi wa uwanja huo. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Rwamlaza alitoa hoja hiyo bungeni alipokuwa akiuliza swali la msingi akitaka kupata ufumbuzi wa jambo hilo ambalo alidai ni la muda mrefu sasa.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kasim Majaliwa, amesema ni kweli shule hizo zipo karibu na uwanja wa ndege.

Amesema shule za msingi Bilele, Tumaini na Zamzam katika manispaa hiyo zipo karibu na kiwanja cha ndege cha Bukoba ambacho kipo katika hatua za ukarabati na ushirikiano wa Benki ya Dunia.

Majaliwa amesema kuwa, mpango wa kuihamisha shule ya msingi Tumaini, tayari halmashauri ya manispaa ya Bukoba imeishatoa kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba 6919.

Amesema shule ya msingi Tumaini itahamishwa katika eneo ilipo mara baada ya ujenzi wa shule mbadala kukamilika katika eneo la Mafumba.

Majaliwa ameeleza kuwa kwa sasa Shirika la ndege litaendelea kuchukua tahadhari za kutosha ili kuhakikisha matumizi ya uwanja hayana madhara kwa wanafunzi.

error: Content is protected !!