August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ruto, Odinga kurusha karata ya mwisho leo

Dk. Wiliam Ruto

Spread the love

 

IKIWA zimesalia siku tatu kabla ya Uchaguzi Mkuu nchini Kenya kufanyika, kampeni za urais nchini humo zinafikia tamati leo Jumamosi huku wagombea wawili wakuu wakitarajiwa kufanya mikutano jijini Nairobi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

William Ruto atakuwa katika uwanja wa Nyayo huku Raila Odinga akimalizia kampeni zake katika uwanja wa Kasarani.

Takriban wapiga kura milioni 22.1 watamchagua mrithi wa rais Uhuru Kenyatta, aliyehudumu tangu mwaka 2013 na ambaye hawezi kuwania muhula wa tatu katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki ambayo demokrasia imekita mizizi.

Kenya yenye makabila 46, inakabiliwa na mfumuko wa bei na hofu ya kujirudia ghasia za baada ya uchaguzi.

Mwaka 2007-2008, zaidi ya watu 1,100 walipoteza maisha katika vurugu za kisiasa na kikabila huku maelfu ya wengine wakilazimika kuyahama makazi yao.

Katika uchaguzi huu, maofisa 150,000 watakuwepo nchini nzima ili kuhakikisha usalama.

error: Content is protected !!