October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ruto, Kenyatta wakutana mara ya kwanza baada ya uchaguzi

Spread the love

RAIS mteule William Ruto leo Jumatatu tarehe 12 Septemba, 2022, amekutana na rais anayeondoka madarakani Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Rais Jijini Nairobi. Anaripotui Mwandishi Wetu…(endelea)

Ruto aliwasili katika Ikulu ya rais saa kumi na kupokewa na mwenyeji wake Uhuru Kenyatta. Rais Mteule aliambatana na mkewe Rachel Ruto.

Hii ni mara ya kwanza kwa wawili hao kukutana tangu Wakenya waliposhiriki katika shughuli ya kupiga kura ili kumchagua rais mpya.

Wawili hao walitofautiana baada ya rais Uhuru Kenyatta kumuunga mkono kiongozi wa upinzani Raila odinga katika uchaguzi uliopita.

Mkutano wao unajiri siku moja kabla ya sherehe ya kumuapisha William Ruto kuwa rais mpya wa Kenya.

Takriban viongozi 20 wa mataifa mbalimbali wamethibitisha kuhudhuria sherehe hiyo hapo kesho Jumanne akiwemo rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Ruto aliibuka mshindi katika uchaguzi wa urais baada ya kumshinda mpinzani wake Raila Odinga.

error: Content is protected !!