Tuesday , 5 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Rushwa ya 100,000 yamponza muuguzi
Habari Mchanganyiko

Rushwa ya 100,000 yamponza muuguzi

Spread the love

RICHARD Zablon, muuguzi katika Zahanati ya Chamwino, jijini Dodoma, leo tarehe 3 Juni 2020 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini humo, kwa tuhuma za kumuomba rushwa ya Sh. 100,000. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) jijini humo imedai, Zablon alimwomba mgonjwa kiasi hicho cha fedha ili ampe huduma ya kusafishwa kizazi.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Sosthenes Kibwengo ambaye ni mkuu wa taasisi hiyo Dodoma amesema, Takukuru imemfungulia mtuhumiwa kesi ya jinai Na. 13/2020 mbele ya Hakimu Paschal Mayumba.

Amesema, anatuhumiwa kuomba rushwa ya Sh. 100,000 na kwamba mpaka anakamatwa, alikuwa tayari amepokea Sh. 60,000.

Kibwengo amesema, mshtakiwa huyo alikamatwa baada ya kugoma kumwachia mgonjwa kisha kwenda naye nyumbani kwake, akishinikiza apatiwe kiasi hicho cha fedha.

“Tarehe 11 Mei 2020, tulipokea taarifa kutoka kwa mwananchi mmoja kwamba, mkewe yupo katika Zahanati ya Chamwino akihitaji huduma ya kusafishwa kizazi, lakini mshtakiwa amehitaji apatiwe fedha ndipo afanye hiyo kazi,” amesema Kibwengo na kuongeza:

“Wakati mtoa taarifa bado yupo ofisini kwetu, mshtakiwa alimpigia simu akisisitiza apewe fedha yake kwa kuwa ameshamsafisha mgonjwa, lakini akaelezwa kwamba amwache mgonjwa aondoke kwani fedha zake atapelekewa.”

Katika hatua nyingine, Kibwengo amesema Takukuru inamshikilia Yusuph Chuma, Mkuu wa Shule ya Msingi Mpamatwa kwa tuhuma za kutumia nyaraka za kughushi ili kutoa Sh. 469,500 kutoka katika akaunti ya shule hiyo.

Chuma anatuhumiwa kwa makosa manne ya kughushi, na kuwasilisha nyaraka zenye maelezo ya uongo juu ya wajumbe wa kamati ya shule hiyo, kwa lengo la kutoa kiasi hicho cha fedha kinyume cha sheria.

“Uchunguzi wetu umeonyesha kwamba Juni mwaka 2019 mtuhumiwa alighushi mihutasari miwili ya vikao vya Kamati ya shule na mkutano wa walimu kuonyesha kwamba waliridhia kiasi cha Sh. 469,500, kitolewe kwenye akaunti ya shule,” amesema Kibwengo na kuongeza:

“Na huku akifahamu kwamba ni uongo na aliwasilisha mihutasari hiyo kwa Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ta Wilaya ya Bahi kwa ajili ya kupata ridhaa yake.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

TMA yaagizwa kutangaza mafanikio yao kikanda, kimataifa

Spread the love  KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara ameiagiza...

Habari Mchanganyiko

NMB yasaidia waathirika wa mafuriko, maporomoko Hanang

Spread the loveWaathirika wa maporomoko ya tope Wilayani Hanang, mkoani Manyara, waliopoteza...

Habari Mchanganyiko

TPF-NET Arusha yaonya jamii ya wafugaji zinazoendeleza ukatili wa watoto na wanawake

Spread the love  MTANDAO wa Polisi wanawake wa Arusha kuelekea siku 12...

Habari Mchanganyiko

Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Greyhorse zasaini mkataba wa bil.7.4

Spread the loveTAASISI ya Mwalimu Nyerere (MNF) imesaini mkataba wa miaka 10...

error: Content is protected !!