Saturday , 13 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Rushwa bado tatizo nchini-Mchungaji
Habari Mchanganyiko

Rushwa bado tatizo nchini-Mchungaji

Rais John Magufuli
Spread the love

ASKOFU wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Kati, Dk. Dikson Chilongani amesema kuwa licha ya kuwa serikali inapambana na rushwa lakini hali hiyo bado ipo na kwa kiwango cha juu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Alitoa kauli hiyo jana katika ibada ya sikukuu ya Kuzaliwa Yesu Kristo iliyofanyika kanisa kuu Jijini Dodoma.

Akihubiri kanisani hapo alisema kuwa ni aibu kwa watumishi wa serikali kuendekeza vitendo vya rushwa licha ya serikali kupiga vita vitendo vya rushwa na ufisadi.

Dk. Chilongani alisema kuwa kwa sasa rushwa zinaendelea kufanyika katika ofisi za Umma huku jina linalotumika kudai rushwa ni “support Docoment” jambo ambalo linakwemisha utendaji wa kazi kwa ufanisi.

“Hivi karibuni nilisafiri kwenda nje ya nacho cha kusikitisha nilipofika uwanja wa ndege wa Dar es saalam, nilipokelewa na wahudumu ambao ni watumishi wa serikali licha ya kuwa sikuwaomba msaada wowote, wa kunisindikiza au kufunga zipu ya begi langu lakini waliniomba hela ya soda ambayo ni rushwa,” alisema Askofu Dk. Chilongani.

Katika mahubiri yake askofu alisema kuwa vita ya rushwa isiwe ya mtu mmoja au serikali pekee bali iwe ya watanzania wote na kama rushwa haitapigwa vita na watu wote ni dhaili kuwawatu wanyonge hawatapata haki zao.

Katika hatua nyingine askofu amekemea baadhi ya askari polisi ambao wanaendekeza vitendo vya rushwa kwani kuendekeza vitendo hivyo ni kupotosha ukweli.

“Rushwa haikuanza leo imekuwepo kwa muda mrefu hata kipindi cha Yesu Yuda aliongwa vipande 30 ili amsaliti Yesu na akafanya hivyo,haikutosha wakati Yesu yupo kaburini alipofufuka askari waliongwa ilibwaseme Yesu akufufuka bali ameibiwa jambo ambalo dhairi lilionekana kuwa ni kupotosha ukweli.

“Kwa mifano hiyo nakemea kabisa vitendo vyote vya rushwa iwe serikalini au katika taasisi mbalimbali kwani rushwa upotosha ukweli na kufanyabhakinisitendeke,” alisema Dk. Chilongani.

Katika hatua nyingine askofu huyo amewataka waumini wa kanisa hilo kwa kuwafikia watu wenye uhitaji badala ya kutumia sikukuu kufanya anasa ikiwemo ulevi na uzinzi.

Alisema wawafikie wahitaji ikiwa ni pamoja na kuwashuhudia neno la Mungu,kuonesha matendo mema ili nao waweze kuonja na kufurahia siku ya kumbukumbu ya kufufuka kwa Yesu Kristo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askofu ataka mafisadi, wauza mihadarati washughulikiwe kumuenzi Sokoine

Spread the love  MHASHAMU Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, Isaac...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mafuriko yaua 33 Morogoro, Pwani

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania imetoa tathmini ya athari ya mafuriko...

Habari Mchanganyiko

Wanafunzi 7 wahofiwa kufariki gari la shule likitumbukia korongoni

Spread the love  WANAFUNZI saba wanahofiwa kupoteza maisha, huku watatu wakinusurika katika...

Habari Mchanganyiko

Wazazi, walezi watakiwa kuwa karibu na watoto wao

Spread the love  WAZAZI na walezi wameagizwa kuwalea watoto wao katika maadili...

error: Content is protected !!