Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Rungwe aelezea machungu Awamu ya Tano “nimeenda Central mara tatu”
HabariHabari za Siasa

Rungwe aelezea machungu Awamu ya Tano “nimeenda Central mara tatu”

Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Rungwe, amedai misingi ya katiba na sheria haikufuatwa katika uongozi wa Awamu ya Tano, na kusema yeye alikwenda katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Rungwe ametoa madai hayo leo Jumatano, tarehe 11 Mei 2022, akizungumza katika kikao cha Baraza Kuu la Chama cha Chadema, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Mwanasiasa huyo amedai kuwa, kama Mungu asingeingilia kati wangepata matatizo makubwa. Hata hivyo, hakufafanua zaidi kuhusu suala ambalo Mungu ameiliingilia kati.

“Katiba iliyopo imeshamwambia Rais wewe hakuna anayekushtaki kwa hiyo fanya unavyotaka, kwa hiyo Rais na ukijakumpata ambaye ana tabia za hovyo kama aliyepita, tunaweza tukajikuta tunapata matatizo makubwa sana labda Mungu aingilie kati, lakini bila yeye tungepata matatizo makubwa sana,” amedai Rungwe.

Rungwe amedai “Ninyi hamjui, mimi nimeshakwenda pale Central mara tatu, mara nne, hamjui ninyi wengine mnasikia jela, jela kuna matatizo.”

Mwenyekiti huyo wa CHAUMMA, amesema chama chake kinataka katiba mpya kwani kinaamini ikipatikana itakuwa suluhu ya sheria zinazolalamikiwa kuna upungufu, ikiwemo Sheria ya Uchaguzi.

“Nyie wote mnajua CHAUMMA kilio chake ni katiba mpya, tunataka katiba mpya hakuna kingine, nafikiri wote tungesimamia hapo sababu hiyo mnasema sheria za uchaguzi zinazaliwa baada ya katiba kuwepo. Sheria za uchaguzi haziji bila katiba kuwepo,” amesema Rungwe na kuongeza:

“Kwa hiyo haya mambo kama hatuelewani wenyewe huku nje sisi sote kwa pamoja, hakuna maana. Wote tungeungana kuwa na katiba mpya ndiyo itatuondolea matatizo tuliyokuwa nayo halafu itafuata sheria za uchaguzi baada ya katiba kupatikana.”

Serikali ya Awamu ya Tano iliyoingia Novemba 2015, ilifika kikomo mwanzoni mwa muhula wake wa pili, Machi 2021, kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wake, Hayati John Magufuli, kilichotokea Hospitali ya Mzena, jijini Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bunge labaini madudu mfumo ukusanyaji mapato, h’shauri tatu kikaangoni

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali...

Habari za Siasa

Mkuu wa wilaya ya Rungwe azindua vyumba sita vya madarasa vya thamani ya 64 mil

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amezindua vyumba...

Habari za Siasa

Mbunge afurahia mabilioni ya Samia kutua jimboni

Spread the love  MBUNGE wa Igunga, Nicholas Ngassa ameishukuru Serikali kwa utekelezaji...

Habari za Siasa

PIC yaishauri Serikali kuanzisha mfuko wa uwekezaji kusaidia mashirika ya umma

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji...

error: Content is protected !!