July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rugemalira aibua mapya sakata la Escrow

Mkurugenzi wa VIP Engineering, James Rugemalira

Spread the love

JAMES Rugemarila, anaendelea kumshawishi Rais Jakaya Kikwete, kutotekeleza maazimio ya Bunge juu ya ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika akaunti ya Escrow. Anatafsiri mazimio ya Bunge kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza ili kutisha wawekezaji na kulichafua bunge, anaandika Saed Kubenea.

Rugemalira ni mmoja wa wamiliki wa kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL). Alikuwa anamiliki asimia 30 ya hisa kupitia kampuni yake ya VIP Engineering Limited.

Kampuni ya Rugemalira, ilichotewa kiasi cha Sh. 105 bilioni kutoka fedha zilizohifadhiwa katika akaunti ya Esvrow.

Katika barua pepe aliyoituma kwa Kikwete,tarehe 29 Novemba 2013, Rugemalira amejenga hoja kadhaa kuhalalisha “wizi” katika akaunti ya Escrow. Hoja hizo ni kama ifuatayo:

 • Kama kuna madai au makosa, katika mchakato wa kumaliza suala la IPTL, walalamikaji wamepewa ruhusu na Jaji John Utamwa kupeleka malalamiko yao mahakamani. Kwa nini hawafanyi hivyo?
 • Ni nani aliyelipa Bunge la Jamhuri mamlaka ya kuamrisha serikali kutaifisha mali ya mtu binafsi bila kupitia njia za sheria?
 • Ni busara Bunge kuamrisha serikali kufuta hukumu ya mahakama, badala ya kuheshimu na kuimarisha utawala wa sheria?
 • Fedha zinaweza kuwa ya Stadard Chartered na wakati huo zikawa za umma?
 • Tanesco inaweza kununua huduma ya umeme kutoka IPTL na badala ya kuilipa IPTL ikajilipa yenyewe?
 • Tangu lini Bunge likawa jukumu la kudai pesa kwa niaba ya kampuni binafsi, wakati kampuni hiyo imefungua madai mahakamani nje ya nchi kwa kisingizio cha kutokuwa na imani na mahakama za Tanzania?
 • Bunge linaweza kuthibitisha kuwa benki ya Standard Chartered (SCB-HK), inadai kampuni yetu deni halali?
 • Bunge letu linapiga kura ya kutokuwa na imani na mahakama iliyoanzishwa kwa mujibu wa katiba?
 • Bunge letu linashabikia mashirika au kampeni za nje au balozi za nje kugonganisha mihimili ya nchi kama Bunge dhidi ya Mahakama?
 • Makosa na madai ya wizi wa VIP au Rugemalira ni kusimamia maslai ya umma katika IPTL?
 • Kama tozo ya uwekezaji wa IPTL ni wizi; je tozo za Songas, Symbion na Aggreko si wizi mkubwa zaidi ambao uchunguzwe kwanza kabla ya huu wa IPTL?
 • Ni halali kwa watu wa nje pamoja na mashirika ya nje na ndani kutoa misaada, lakini ni haramu kwa VIP au James Rugemalira kutoa misaada?
 • Kuna watu wengi na asasi nyingi za kiraa zimepokea fedha kutoka kwa watu binafsi au taasisi za nje?
 • Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), aliandika katika ripoti yake kwamba anachukua nafasi ya Mahakama Kuu na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ni “Mahakama ya Rufaa.”
 • Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), ina uhalali wa kutoza kodi kwenye fedha zinazo daiwa kuwa za wizi?
error: Content is protected !!