October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rugemalira aachiwa huru

Spread the love

 

MFANYABIASHARA James Rugemalira leo tarehe 16 Septemba, 2021 ameachiwa huru Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kufuta mashtaka yaliyokuwa yanamkabili tangu Juni 2017. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wakili wa Serikali mwandamizi, Grace Mwanga amedai upande wa mashtaka hawana nia ya kuendelea na shauri hilo chini kifungu cha 91(1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya mwaka 2019.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alikubali ombi lililotolewa na upande wa jamhuri na kumuachia Rugemalira.

“Kesi naiahirisha hadi Desemba 23, 2021 na mshtakiwa Makandege ataendelea kuwa mahabusu,” amesema hakimu huyo.

Rugemalira, mwanasheria wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Joseph Makandege, Mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Harbinder Seth (63), tarehe 19 Juni, 2017 walifikishwa Mahakamani hapo na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) wakishtakiwa kwa makosa 6 ya uhujumu uchumi.

Katika kesi ya msingi, Rugemalira wenzake walikuwa wanakabiliwa na makosa ya kughushi, kuongoza genge la uhalifu, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 22.19 na zaidi ya Sh bilioni 309.46.

Walidaiwa kutenda makosa hayo, tarehe 18 Oktoba, 2011 na tarehe 19 Machi, 2014 jijini Dar es Salaam walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ili kutenda kosa.

Mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Harbinder Seth (63) alikiri mashtaka yake na kuachiwa Juni mwaka huu na mahakama hiyo baada ya kuhukumiwa kulipa Sh bilioni 26.9 baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia Sh309 bilioni kwa njia ya udanganyifu.

 

Pia, mahakama hiyo imemhukumu kifungo cha nje cha mwaka mmoja akitakiwa kutokujihusisha makosa yoyote ya jinai.

error: Content is protected !!