Tuesday , 23 April 2024
Home Kitengo Michezo Ruge amponza Dudubaya, Waziri atoa maagizo mazito
Michezo

Ruge amponza Dudubaya, Waziri atoa maagizo mazito

Godfrey Tumaini 'Dudubaya'
Spread the love

HARRISON Mwakyembe, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo ameliagiza Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), kumchukulia hatua msanii, Godfrey Tumaini maarufu kama ‘Dudubaya’, kwa kumdhihaki aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vipindi wa Clouds Media Group, marehemu Ruge Mutahaba. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Mwakyembe ametoa agizo hilo leo tarehe 27 Februari 2019, baada ya Dudu Baya kusambaza video katika mitandao ya kijamii inayomuonyesha akimdhihaki marehemu Ruge.

Aidha, Mwakyembe ameitaka BASATA kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kumchukulia hatua za kisheria Dudubaya kufuatia hatua yake hiyo.

Saa chache baada ya Mwakyembe kutoa agizo hilo, Dudubaya amemjibu akisema kuwa, bora mafuta  yatakayotumika kwenye difenda kwenda kumkamata, bora yakakamate majambazi kwa kuwa yeye yuko tayari kwenda katika kituo chochote atakachoelekezwa na Jeshi la Polisi kwenda.

“Niko ‘home’ nyumbani mheshimiwa Mwakyembe umeagiza nikamatwe na jeshi la polisi, usisumbue madifenda kupoteza mafuta bora kakamate majambazi, waambie polisi waniite kituo gani kama ni Oysterbay, Salender Bridge,  central au Mabatini ‘im raedy to come there, thisi is God is job,” amesema Dudubaya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

Michezo

Ujanja ni kubeti na Meridianbet

Spread the love  JUMAPILI ya leo imekaa kihela hela sana ndani ya...

Michezo

Anza Jumamosi yako na mkwanja wa Meridianbet

Spread the loveJumamosi ya leo ODDS zimekaa kijanja sana ndani ya Meridianbet...

error: Content is protected !!