Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari Rufaa za kina Mdee zatupwa, Mbowe asema…
HabariHabari za SiasaTangulizi

Rufaa za kina Mdee zatupwa, Mbowe asema…

Spread the love

 

RUFAA za Halima Mdee na wenzake 18 za kupingwa kufukuzwa uanachama na kamati kuu ya Chadema zimetupiliwa mbali na wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ni leo Alhamisi saa 7:00 usiku katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo Mdee aliwaongoza wenzake kwenda kusikiliza rufaa hizo.

Baada ya wajumbe hao chini ya Mwenyekiti, Freeman Mbowe kusikiliza rufaa hizo walizoziwasilisha ofisi ya Katibu Mkuu, Joh Mnyika, Mbowe alizungumza.

Pamoja na mambo mengine, Mbowe aligusia jinsi alivyotaka kuwasaidia wakati sakata lao la kusaliti, kughushi na kujipeleka bungeni kujiapisha kuwa wabunge wa viti maalum.

Mbowe alisema aliwasiliana na wazazi wa Halima ili wamsihi mtoto wao juu ya uamuzi alioufanya lakini ikashindikana.

“Nilipokuwa gerezani nilimwomba katibu mkuu (John Mnyika) amlete Halima, alikuja na (Ester Bulaya, niliwahisii sana.”

Akizungumza kwa uchungu, Mbowe amesema”niliwauliza nani aliwadanganya? Acheni huu ujinga!Nilimwambia kama unataka kazi niambiee nitakutafutia kazi hata nje ya nchi, utalipwa vizuri achana na ubunge.Nipo gerezani namuwaza Halima.”

Baada ya maelezo hayo, Mbowe aliwaongoza wajumbe wa kikao hicho kupiga kura kwa za wazi kwa kanda moja moja kwa wale wanaokubalia a na rufaa hizo ama kuzipinga.

Mwisho wa kura hizo, wajumbe walizitupilia mbali hivyo kuhitimisha suala hilo la uanachama ndani ya Chadema.

Kwa uamuzi huo wa Baraza Kuu na kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Mdee na wenzake 18 wamepoteza sifa za kuwa wabunge wa Bunge la Tanzania.

Aidha, Mdee na wenzake wanayo fursa ya kwenda kupinga uamuzi huo wa Chadema Mahakamani ikiwa wana dhamira hiyo.

Mbali na Mdee aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la wanawake wa Chadema (Bawacha), wengine ni, waliokuwa wajumbe wa Kamati Kuu, Ester Bulaya na Esther Matiko pamoja na aliyekuwa katibu mkuu wa Bawacha, Grace Tendega.

Pia wamo, Hawa Mwaifunga, aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Bawacha (Bara); Agnesta Lambat, aliyekuwa katibu mwenezi na Asia Mwadin Mohamed, aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Bawacha Zanzibar na Katibu Mkuu, Bawacha-Bara, Jesca Kishoa

Wengine ni, aliyekuwa katibu mkuu wa Baraza la Vijana (Bavicha), Nusrat Hanje, aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoani Mtwara, Tunza Malapo.

Cecilia Pareso, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Salome Makamba, Anatropia Theonest, Conchesta Lwamlaza, Felister Njau na Stella Siyao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!