Saturday , 10 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rufaa yawakwamisha Mbowe, Matiko
Habari za Siasa

Rufaa yawakwamisha Mbowe, Matiko

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko wakiwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam
Spread the love

UAMUZI wa Rufani ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (Chadema)-Taifa na Ester Matiko, Mbunge wa Tarime vijijini umekwamisha usikilizwaji wa kesi ya uchochezi inayowakabili kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Washtakiwa wengine kwenye kesi hiyo ni pamoja na Dk. Vicent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema; Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa mjini; John Mnyika, Mbunge wa Kibamba; Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda; Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini na Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar.

Leo tarehe 14 Februari 2019 Kelvin Mhina, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo amesema kuwa, mahakama hiyo inasubiri uamuzi wa mahakama ya rufani ili kesi hiyo ipangiwe hakimu mpya kwenye.

Amesema kuwa, hawajampangia hakimu yoyote mpaka watakapopata majalada ya maamuzi kutoka Mahakama ya Rufaa.

Kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwe na Jaji Wilbard Mashauri kwa sasa ambaye alikuwa Hakimu Mkazi kwenye mahakama hiyo.

Ester Martin, Wakili wa Serikali, amedai kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba, wanasubiri uamuzi wa Mahakama ya Rufaa.

Wakili wa Utetezi, Profesa Abdallah Safari alidai hawana pingamizi na kwamba, rufani iliyotolewa na upande wa mashitaka Mahakama ya Rufaa itasikilizwa tarehe 18 Februari 2019.

Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi 28 Februari 2019kwa ajili ya kutajwa.

Tarehe 23 Novemba 2018 Jaji Wilbard Mashauri akiwa Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, alifuta dhamana kwa Mbowe na Matiko kutokana na kukiuka masharti yake (dhamana).

Baada ya uamuzi huo, washitakiwa hao wakiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala, walikata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa mahakama hiyo ya kufuta dhamana.

Mahakama Kuu chini ya Jaji Sam Rumanyika baada ya kusikiliza pingamizi kwa pande zote, iliamua kuanza usikilizaji wa rufaa hiyo.

Upande wa serikali ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi ulidai kuwa, wamekata rufaa katika Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi uliyotolewa na kuiomba mahakama hiyo kuacha kuendelea kusikiliza rufaa hiyo kwa sababu haina mamlaka.

Baada ya upande wa serikali kuwasilisha rufaa yao,  kuliibuka malumbano ya kisheria baina ya mawakili wa pande zote, huku mawakili wa kina Mbowe wakiongozwa na Wakili Kibatala, walipinga uhalali wa taarifa ya serikali ya kusudio la kukata rufaa kwa madai, hawajafahamishwa na Msajili wa Mahakama Kuu kuhusu kuwepo kwa taarifa hiyo.

Katika kesi ya msingi, washitakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari Mosi na 16, mwaka  2018 maeneo ya Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!