Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rufaa ya Sabaya, wenzake Februari 2022
Habari za SiasaTangulizi

Rufaa ya Sabaya, wenzake Februari 2022

Lengai Ole Sabaya akiwa mahakamani Arusha
Spread the love

 

RUFAA ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai ole Sabaya na wenzake wawili imepangwa kusikilizwa tarehe 14 Februari 2022, Mahakama Kuu Kanda ya Arusha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Ruth Massam amepanga tarehe hiyo ya kuanza kusikilizwa kwa rufaa hiyo namba 129/2021, baada ya shauri hilo kufika mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

Alieleza kuwa siku hiyo shauri hilo litafika mbele ya Jaji atakayepangiwa kuanza kulisikiliza mfululizo kama itakavyoelekezwa.

Awali, Wakili wa waleta rufaa, Moses Mahuna aliieleza Mahakama kuwa shauri hilo limekuja kutajwa na wako tayari kupokea amri zingine za Mahakama.

Kwa upande wa wajibu rufaa, Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka alieleza kuwa wako tayari na wanaomba tarehe na wakati mwafaka kwa ajili ya kusikiliza shauri hilo.

Kwenye shauri hilo, Sabaya na wenzake wawili, Sylvester Nyegu na Daniel Bura wanapinga uamuzi uliotolewa kwenye kesi ya jinai namba 105/2021.

Kesi hiyo ilisikilizwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo ambapo tarehe 15 Oktoba 2021, walihukumiwa kifungo cha miaka 90 jela kwa makosa matatu waliyokutwa na hatia.

Mahakama hiyo iliamua adhabu hiyo iende kwa pamoja, hivyo kila mmoja anatumikia kifungo cha miaka 30 jela.

Lengai Ole Sabaya akiwa mahakamani Arusha

Mahakama iliwatia hatiani kwa makosa matatu tofauti ya unyang’anyi wa kutumia nguvu na unyang’anyi wa kutumia silaha.

Hakimu Amworo, alitoa adhabu hiyo tarehe 15 Oktoba, saa 11:47 jioni baada ya kuanza kusoma hukumu hiyo saa 5:56 adhuhuri.

“Kama alivyosema Wakili wa Serikali Mwandamizi, Felix Kwetukia kwamba mshitakiwa wa kwanza Lengai ole Sabaya alikuwa Mkuu wa Wilaya aliyeteuliwa na Rais, kitendo alichofanya kinadhalilisha taasisi ya Rais,” alisema Hakimu huyo na kuongeza:

“Na hakuna ubishi, kwamba wote ni vijana na wanahitajika kama walivyoeleza mawakili wao, na kwa mujibu wa sheria, hakuna ubishi kwamba mikono yangu imefungwa, naweza kuwafunga miaka 100, lakini kurudi chini siruhusiwi kufunga chini ya miaka 30.

“Mbali ya kwamba Wakili wa Serikali ameomba wachapwe viboko na walistahili wachapwe, maana yake nao walikuwa wanawatoa wenzao wenge.

“Lakini mawakili wenzetu wameshindwa kuinyambulisha sheria ya zamani ya watoto waliokuwa wanapigwa viboko, lakini sheria mpya hawapigwi viboko, wamepenyea hapo angalau. Basi mikono yangu imefungwa adhabu ya chini ni miaka 30 na viboko.

“Kosa la kwanza kila mshitakiwa atatumikia miaka 30, kosa la pili miaka 30 kila mmoja na la tatu miaka 30 kila mmoja, kwa viboko mawakili wameshinda, sitatoa viboko na adhabu ziende pamoja. Mna haki ya kukata rufaa, iko wazi.”

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!