January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RPC Dar: Suala la Askofu Mwingira linashughulikiwa makao makuu

Askofu wa Kanisa la Efatha, Josephat Mwingira

Spread the love

 

SAKATA la kuhojiwa Askofu wa Kanisa la Efatha, Josephat Mwingira, juu ya madai yake ya kwamba alinusurika kuuawa na watu wa Serikali, mara tatu, linashughulikiwa na Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea.

Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa, tarehe 31 Desemba 2021 na Kamanda wa Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Jumanne Muliro, alipoulizwa na wanahabari hatua iliyofikiwa katika uchunguzi wa suala hilo.

“Shauri linaendelea vizuri na kwa kifupi sana, linashughulikiwa na Polisi makao makuu,” amesema ACP Muliro.

Sakata hilo liliibuka hivi karibuni, baada ya Askofu Mwingira kupitia mahubiri yake yaliyorushwa mubashara na Kituo cha Televisheni cha Star Tv, kutoa tuhuma nzito dhidi ya Serikali.

Katika tuhuma hizo, Askofu Mwingira alidai alinusurika kuuawa na watu wa Serikali mara tatu, dereva wake alihusishwa katika mauaji ambayo hakuyataja.

Pia, alidai dada ambaye hakumtaja jina, aliyetoa taarifa za mipango ya yeye kuuawa, aliuliwa akiwa kwenye Hotelki ya Rombo, Shekilango, mkoani Dar es Salaa.

Kufuatia tuhuma hizo nzito zilizoibua sintofahamu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, aliagiza Jeshi la Polisi limhoji kiongozi huyo wa kiroho ili kufanyia kazi malalamiko yake.

error: Content is protected !!