November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RPC Dar apewa rungu kumsaka, kumhoji Askofu Mwingira

Askofu wa Kanisa la Efatha, Josephat Mwingira

Spread the love

 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, George Simbachawene ameliagiza Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kumtafuta na kumhoji Askofu wa Kanisa la Efatha, Josephat Mwingira kuhusu “tuhuma nzito sana alizozitoa.” Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ni baada ya Askofu Mwingira kutumia mahubiri ya jana Jumapili, tarehe 26 Desemba 2021 ya sikukuu ya Krismasi, katika Kanisa la Efatha Mwenge jijini humo, kutoa tuhuma mbalimbali ikiwemo ya kunusurika kwake kuuawa mara tatu na watu wa Serikali.

Leo Jumatatu, tarehe 27 Desemba 2021, katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri Simbachawene ameulizwa na waandishi kuhusu tuhuma hizo na hatua zinazochukuliwa.

Akijibu swali hilo, Waziri Simbachawene amesema, “hili ambalo limesikika siku hizi mbili za Krismas, limetamkwa na Askofu Mwingira, na mimi nimeliona mitanmdaoni.”

“Nimepata ile ‘clip’ lakini kama haina sauti, sijaisikia vizuri na bado tunaendelea kulifuatilia, ni tuhuma nzito sana, linapotolewa na kiongozi wa kijamii wa dini na kiongozi maarufu anayejulikana.”

“Kama matukio yote yalikuwa yanatokea, tunapata shida kidogo, kwa nini alikuwa hatoi taarifa kwenye vyombo kama polisi ili hatua ziweze kuchukuliwa ili kuwatafuta wahusika, lakini yote haya yatokee, yatokee, yatokee unakaa kimya, unasubiri Krisimas ya mwaka 2021 halafu unasukua lawama zote hizi,” amesema

Waziri huyo amesema, “kama aliyoyasema yatakuwa ni kweli, tutahitaji atusaidie kutupa taarifa zaidi na kwa kuwa tunautafuta uhalisia, si vibaya RPC wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kumtafuta ili kupata ukweli zaidi kwani pale alikuwa anaongea na waumini.”

“Nchi yetu inaongozwa na utawala wa haki na sheria, mtu hawezi kukaa akiwa na hofu na maisha yake na akaenda kusema kama alivyofanya. Tunahitaji kupata zaidi na zaidi ili kuchukua maelezo ya kutosha ili tuweze kushughulika na hao aliowaita,” amesema.

error: Content is protected !!