Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Royal Tour kufufua hoteli za kitalii nchini
Habari Mchanganyiko

Royal Tour kufufua hoteli za kitalii nchini

Spread the love

SERIKALI imesema katika kuhakikisha matokeo chanya ya Filamu ya Royal Tour yanaonekana wanahakikisha wanazungumza na wawekezaji na wadau wa ya sekta ya utalii ili waweze kufufua hoteli za kitalii ambazo zimefungwa. Anaripoti Selemani Msuya, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamesemwa leo tarehe 12 Mei, 2022 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda Prof. Godius Kahyarara wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari walioshiriki Mkutano wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu jijini Dar es Salaam.

Amesema Royal Tour itachangia ongezeko la wafanyabiashara, wawekezaji na watalii, hivyo wao kama Serikali wanawajibu wa kuweka mazingira rafiki ambayo yatawezesha mwitikio huo haupati vikawzo wanapokuja nchini.

“Leo tuna kikao na wadau wa sekta ya utalii, wawekezaji na wafanyabiashara ambapo mazungumzo yatajikita ni kwa namna gani wana utayari wa kushirikiana na sisi kuchochea sekta ya utalii.

“Zipo hoteli za kitalii ambazo zilifungwa, tunataka zifufuliwe, lakini kuna Shirika la Umma la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), wana majengo mengi ambayo ndani yake yana hoteli za nyota tano, wote hawa tukikaa na kujadiliana tutapata muafaka,” amesema.

Amesema pia ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Marekani mikataba yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 5.4 imesainiwa na matokeo yake yanatakiwa yatumike kuwekeza nchini na sekta ya utalii ni mojawapo.

Prof. Kahyarara amesema imani yao ni kupitia Royal Tour Tanzania itapokea watalii milioni 5 ifikapo mwaka 2025, hali ambayo itachangia ukuaji wa uchumi na kuchochea maendeleo.

Aidha, katibu mkuu huyo amesema katika mkataba ambayo wamesaini nchini Marekani wanatarajia kuwepo ndege moja kwa moja kutoka jiji la Dallas hadi Tanzania moja kwa moja.

“Tumejiandaa vizuri kuhakikisha Royal Tour inafanya mapinduzi makubwa nchini, ili Tanzania iweze kupaaa kiuchumi,” amesema.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Amos Nnko amesema wao kama bodi wanaendelea kushirikiana na sekta ya utalii kuhakikisha hakuna kikwazo kinatokea pale ambapo kasi ya watalii itaongezeka.

Nnko amesema sekta hiyo imefanya marekebisho ya miundombinu mbalimbali kwenye sehemu za utalii kupitia fedha za mkopo usio na riba wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Sh. trilioni 1.3.

“Tunashirikiana na wadau wa utalii kupitia Shirikisho la Watoa Huduma za Utalii (TCT), hivyo ni matumanini yetu tutaenda sawa kwa maslahi ya nchi,” amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Royal Tour ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Hassan Abbas amesema filamu hiyo imeanza kuonesha matokeo chanya kwa nchini tangu kuzinduliwa kwake.

Amesema matokeo ya Royal Tour itakuwa sehemu ya mchango mkubwa wa mikakati ya nchi iliyopo, hivyo kuwataka Watanzania waendelee kuiunga mkono, huku akisema kipande kilichooneshwa ni sehemu kidogo ya filamu yote.

“Royal Tour imeoneshwa kwenye vituo vya televisheni zaidi ya 300 nchini Marekani pekee, ila kwenye mitandao mingi pia inaonekana. Kusema kweli manufaa ni makubwa ikiwemo Rais Samia kukuta na wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa zaidi ya 40 wa sekta ya filamu, utalii na nyingine,” amesema.

Kwa upande wale Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula amesema Tanzania inaendelea kufunguka ambapo alitolea mfano bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga kuwa wapo katika hatua nzuri za utekelezaji.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus amesema kwa ujumla ziara ya Raisa Samia katika nchi ya Marekani na Uganda imekuwa na matokeo mazuzi katika sekta zote ambazo wamefanya majadiliano.

Yunus amesema matarajio yao ni ziara hizo kuchangia ongezeko la ajira 300,000 kwa kada mbalimbali ikiwemo utalii, miundombinu, afya, elimu na nyingine nyingi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

error: Content is protected !!