July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rotary Club yaikabili Maleria Arusha

Maji yaliyotuama ni chanzo cha mazalia ya mbu

Spread the love

CHAMA cha kujitolea cha Rotary Club Sunrise kimetoa msaada wa vifaa vya kisasa pamoja na dawa za kuharibu mazalia ya mbu katika Kata ya Elerai, Arusha. Anaandika Ferdinand Shayo, Arusha …(endelea).

Jitihada hizo zinafanywa ili kukabiliana na ugonjwa wa malaria ambao bado ni tatizo kubwa katika jamii.

Katibu wa Rotary, Haji Abdully amesema kuwa, zoezi la kuharibu mazalia ya mbu katika madimbwi ya maji, vichaka na maji yaliyotuama na maeneo mengine litasaidia kupunguza athari za kiafya na kiuchumi zinazosababishwa na ugonjwa huo.

Haji amesema, wagonjwa wa malaria ni wengi katika vituo vya afya hivyo jitihada hizo zitapunguza msongamano wa wagonjwa katika zahanati na hospitali .

“Miezi miwili iliyopita tulitoa vyandarua kwa watu wasiojiweza na kwa sasa tunaendelea na juhudi hizi endelevu za mradi wetu wa malaria na leo pia tumekabidhi baiskeli ya mlemavu kwa mama mmoja ili kuigusa jami kwa namna tofauti.

“Tunawakaribisha Watanzania wengine wajiunge nasi katika kujitolea si lazima uwe na fedha nyingi kwani kutoa ni moyo,” amesema Haji.

Diwani wa Kata ya Elerai, anayemaliza muda wake Injinia Jeremiah Mpinga amesema, vita dhidi ya malaria ni ya dunia nzima na kuwataka Watanzania na wadau wengine kujitokeza kuisaidia jamii kupambana na ugonjwa huo.

Mpinga amesema kuwa, Rotary wamekua mfano wa kuigwa kutokana na kuwa sehemu ya utatuzi ya matatizo ya Watanzania hasa wananchi wa kata ya Elerai na Arusha kwa ujumla.

Amesema kuwa, Rotary wamemsaidia mama aliyekua na mlemavu wa miguu kwa zaidi ya miaka 10 kwa kumpatia baiskeli maalumu ya kutembelea.

 

error: Content is protected !!