May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rose Muhando: Nataka mume mzungu mwenye pesa

Spread the love

 

MSANII wa muziki wa Injili nchini, Rose muhando amefunguka kwamba mojawapo ya mambo anayotaka afanikiwe kwa mwaka huu ni kumpata mume mzungu mwenye mapene. Anaripoti Mwandishi Wet… (endelea)

Kupitia ukurusa wake wa Instagram alifichua kwamba anafurahi maisha anayoishi na amejitolea katika huduma yake ya injili na mara nyingi husafiri kueneza injili, kutokana na hilo anasema ni vigumu kutulia kwenye ndoa.

Aidha, amesema kuolewa kutarudisha huduma yake nyuma, hivyo hayuko tayari kuingia kwenye ndoa.

Muhando ambaye ni mama wa watoto watatu anasema anataka mwanamume mzungu mwenye pesa.

“Yesu nitendee.. Ombi langu mwaka huu nataka nipate mume mzungu na mwenye ela” alisema Rose Muhando.

Isitoshe aliwambia mashabiki wake wanaweza kutuma maombi yao kwa chochote wangetaka Mungu awatendee mwaka huu na angewasaidia kwa maombi.

“Unaweza nitumia na wewe challenge yako ya Ombi lako huku ukiandika ombi lako unalotaka Mungu akufanyie mwaka huu 2022” alidokeza.

error: Content is protected !!