August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ronaldo, Raniel watamba tuzo za FIFA

Washindi wa Tuzo za FIFA

Spread the love

HATIMAYE washindi katika tuzo za FIFA (The FIFA best Awards) wamefahamika jana katika hafla iliyofanyika Zurich, huku Cristiano Ronaldo akiibuka kuwa mchezaji bora wa mwaka na Claudio Raniel akichukua tuzo ya kocha bora wa mwaka, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Ronaldo ameshinda tuzo hiyo baada ya kuwashinda Lionel Messi kutoka Fc Barcelona na Antoine Griezmann wa Atleticol Madrid, kutokana na kuwa na mafanikio makubwa katika msimu uliomalizika kwa ngazi ya klabu na timu ya taifa.

Hii itakuwa tuzo ya tatu kubwa kwa Ronaldo toka kumalizika kwa msimu 2015/16 baada ya kushinda tuzo ya Mchezaji bora wa Ulaya, Ballon d’Or na hii ya mchezaji bora wa FIFA na kuwa mchezaji mwenye mafanikio makubwa ndani na nje ya uwanja kwa mwaka 2016.

Lakini pia katika hafla hiyo kocha wa klabu ya Leicester City inayoshiriki ligi kuu nchini England Claudio Raniel alifanikiwa kutwaa tuzo ya kocha bora wa mwaka, baada ya kufanikiwa kuongoza kikosi chake kushinda ubingwa wa ligi kuu na kuifikisha timu hiyo katika hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Raniel amewabwaga makocha Fernando Santos aliyefanikiwa kuiongoza Ureno kuchukua ubingwa wa kombe la Euro, Zinedine Zidane aliyechukua kombe la ligi ya mabingwa ulaya akiwa na Real Madrid, makocha wengine waliokuwa katika kinyang’anyiro hicho hapo awali ni Pep Guardiola, Chris Coleman, Didier Deschamps,Diego Simeone, Luis Enrique, Mauricio Pochettino na Jürgen Klopp.

error: Content is protected !!