July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ronaldo, Donnarumma watamba Tuzo Euro

Cristiano Ronaldo

Spread the love

STAA na Nahodha wa timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, pamoja na mlinda mlango wa timu ya Taifa ya Italia, Gianluigi Donnarumma, wamejinyakuliwa tuzo binafsi mara baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Euro, mwaka huu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Michuano hiyo ilikamlika jana, kwa Timu ya Taifa ya Italia kuibuka mabingwa baada ya kupata ushindi wa penalti 3-2, dhidi ya Uingereza, kwenye mchezo uliofanyika uwanja wa Wembley, London.

Ndani ya dakika 90 timu hizo zilifungana bao 1-1, huku Uingereza wakiwa wa kwanza kupata bao kwenye dakika ya pili kupitia kwa Luke Shaw, na kwenye dakika ya 67, mlinzi wa kati wa Italia, Leonardo Bonucci alisawazisha bao hilo.

Licha ya timu yake kutolewa kwenye hatua ya 16 bora, Ronaldo ameibuka kuwa kinara wa upachikaji mabao kwenye michuano hiyo, baada ya kufunga mabao matano, sawa na mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Jamhuri ya Czech Patrik Schick.

Gianluigi Donnarumma

Wawili hao wamefungana kwa mabao, lakini Ronaldo amepewa kiatu hiko, kufuatia kutoa pasi moja (assist) iliyoazaa bao.

Aidha sababu nyingine ya Ronaldo kupewa tuzo hiyo ya ufungaji bora ni baada ya kupachika mabao hayo matano katika michezo minne, tofauti na Schick aliyepachika mabao hayo kwenye michezo mitano.

Tuzo ya mchezaji bora wa michuano hiyo kwa mwaka huu ilienda kwa mlinda mlango wa Italia, Donnarumma, ambaye kwenye mchezo huo wa fainali aliiibuka shujaa mara baada ya kudaka penalti mbili zilizopigwa na Bukayo Saka, pamoja na Jodarn Sancho.

Mlinda mlango huyo katika michuano hii amecheza michezo yote, huku akiwa hajawahi kuruhusu mabao zaidi ya mawili langoni mwake.

Pedro Gonzalez ‘Pedri’

Tuzo nyingine ya mchezaji kijana ilikwenda kwa kinda la Timu ya Taifa ya Hispania, Pedro Gonzalez ‘Pedri’ ambaye anakipiga kwenye klabu ya FC Barcelona, na kwenye michuano hii amecheza jumla ya michezo sita.

Katika michuano hiyo timu za Italia na Hispania ndiyo zimeonekana kuwa na safu bora ya ushambuliaji mara baada ya zote kupachika mabao 13.

Licha ya kupoteza fainali Uingereza imeibuka kuwa timu yenye safu bora ya ulinzi baada ya kuruhusu mabao 2, kwenye michezo saba.

error: Content is protected !!